DIAMOND: NINA HOFU YA KUNYANG'ANYWA TIFFAH


Musa mateja


Kazi ipo! ‘Kichaa’ wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, amekumbwa na hofu ya kunyang’anywa mwanaye anayemuita malkia, Latifah Nasibu ‘Princes Tiffah’ baada ya mama mtoto wake, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ kutimka naye kwenda kwao nchini Afrika Kusini ‘Sauz’.


Latifah Nasibu ‘Princes Tiffah’.

Habari kutoka ndani ya familia ya staa huyo zilieleza kwamba, wikiendi iliyopita Diamond alisikika akiwaambia jamaa zake kuwa ana hofu hiyo na kwamba haamini kabisa kuondoka kwa Zari na Tiffah kwani anahisi huko aliko maadui zake wanaweza kumteka mwanaye kwa kuwa siku zote wamekuwa wakiongea maneno machafu.

“Alikuwa amekaa na washikaji zake na mimi nilikuwepo, alikuwa anatia huruma kweli maana tulikuwa tukipiga stori mara ghafla nikamuona amechenji baada ya kumuuliza akaniambia anamuwazia sana mwanaye Tiffah huko South kwani anahisi uwepo wake kule anaweza kutekwa na kujikuta akifanyiwa mambo yasiyokuwa sawa na baadhi ya wabaya wake ambao wamekuwa wakimuombea mabaya kila kukicha.

“Diamond anasema hana amani sana kwani amekuwa akimuomba Zari asiende hadi mtoto afikishe angalau miezi tisa lakini amegoma kufuatia miradi yake kuyumba kwani amekuwa mbali nayo kwa muda mrefu.


‘Kichaa’ wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’.

“Unajua Zari amekaa miezi mingi sana tangu alipotimba Bongo kujifungua, ungekuwa uwezo wake na si sheria za nchi angefanya kila liwezekanalo amhamishie huku maana hafurahishwi na kitendo cha kuwa mbali na mwanaye Tiffa,” kilisema chanzo hicho na kuongeza:

“Unajua Ivan (aliyekuwa mume wa Zari aliyezaa naye watoto watatu wa kiume) huwa anakwenda kwa Zari na yule shwahiba wake, King Lawrence ‘so’ lolote laweza kutokea kwani mara kwa mara walishasema kuwa Tiffah ni damu yao hadi wakataka akapimwe DNA.”

Akizungumza na Ijumaa Wikienda, Diamond alikiri kupatwa na hofu hiyo kwani hana imani sana na jamaa hao.
“Mimi kama binadamu lazima niwe na hofu na mwanangu hasa linapokuja suala la kuwa mbali na mimi na ndiye mtoto wangu wa kwanza hivyo lazima niwaze,” alifunguka Diamond

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini