JOKATE KIDOTI, ALIKIBA Gumzo!

MASTAA wa Bongo Fleva, Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ na mkali wa kibao cha Chekecha Cheketua, Ali Saleh Kiba ‘King Kiba’, juzikati waligeuka kivutio ndani ya Uwanja wa Taifa, Dar mara baada ya kuwasili wakiwa katika pozi la kimahaba, pasipo kujali macho kodo ya mashabiki wa soka waliofurika uwanjani hapo. 
Mastaa wa Bongo Fleva, Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ na Ali Saleh Kiba ‘King Kiba’
 Tukio hilo lilijiri Septemba 26, mwaka huu ambapo wawili hao walikuwa wameenda uwanjani hapo… …kushuhudia mechi ya watani wa jadi, Yanga na Simba.Wawili hao wakiwa wameshikana kimapenzi bila wasiwasi walijumuika pamoja na mashabiki wengine wa Yanga kuishangilia timu yao ambayo iliibuka kidedea kwa ushindi wa mabao 2-0. 

Mmoja wa mashabiki wa Ali Kiba alisema hiyo ilikuwa ni mara yake ya kwanza kuwaona wakiwa pamoja na kwa kweli walikuwa kivutio kikubwa kwake, kwani walikuwa kama mke na mume, tena sehemu kama ile.
“Kiukweli leo ni siku yangu ya furaha kwa kuwa timu yangu imeshinda, ila kivutio kikubwa nimekipata kutoka kwa Ali Kiba na Jokate, maana sijawahi kuwaza hata siku moja kama hawa jamaa wangeweza kuambatana hadi uwanjani, maana nimezoea kumuona Kiba pekee ila leo kwangu imeniongezea furaha kwa kuwa namkubali King Kiba,” alisema shabiki huyo.
 Kabla ya siku hiyo, kulikuwa na tetesi za wawili hao kukwaruzana, kwa kile kinachodaiwa kuwa Jokate kukerwa na picha ya mtoto wa Kiba aliyezaa na mwanamke mwingine ambayo aliiweka kwenye ukurasa wake wa Instagram

Hata hivyo, inasemekana kuwa bifu hilo limemalizika kama meneja wa msanii huyo, Bude alivyothibitisha. “Ni kweli kulikuwa na tofauti kidogo lakini hivi sasa wapo pamoja.”
 Jokate alipoulizwa kuhusu picha iliyowaonesha wakiwa wameshikana ndani ya uwanja huo, hakusema kitu badala yake, alirejesha jibu lenye alama ya mdomo unaobusu, kuonesha kuwa ni upendo tu!

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini