KIMENUKA! SIMBA SC Yamshtaki Donald NGOMA wa YANGA SC, TFF

DONALD NGOMA

Fowadi wa Yanga, Donald Ngoma.
 Nicodemus Jonas, Dar es Salaam
UONGOZI wa Simba umeliandikia barua Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kushtaki kitendo cha fowadi wa Yanga, Donald Ngoma kumpiga kichwa beki wao, Hassan Kessy makusudi, katika mchezo wa wikiendi iliyopita ambao Yanga walishinda mabao 2-0.

 Simba wameamua kupeleka malalamiko yao TFF pamoja na nakala ya barua hiyo kwa Bodi ya Ligi wakipinga maamuzi ya mchezo huo ambao wanaamini ulikuwa na upungufu mkubwa.
 Msemaji wa timu hiyo, Haji Manara, ameliambia Championi Jumatano kuwa, barua hiyo waliiwasilisha tangu juzi Jumatatu, hivyo wanasubiria majibu.
“Kikubwa katika barua yetu tumebainisha upungufu uliojionyesha kwenye mchezo ule, Ngoma alionekana kumpiga kichwa Kessy pasipokuwa na mpira lakini refa hakuchukua hatua yoyote. 
Pia mwamuzi mwenyewe (Israel Nkongo) alikuwa akiwatukana wachezaji wetu matusi, sasa tunataka TFF waliangalie suala hili kwa mapana yake,” alisema Manara.
 Katibu wa TFF, Selestine Mwesigwa, alipotafutwa alisema: “Bahati mbaya kiutawala siruhusiwi kuzungumzia masuala ya barua au malalamiko kama imefika ama haijafika mezani kwangu, lakini kama kuna ishu kutoka kwao tutaiona.”
 Katika michuano ya Kombe la Kagame, Ngoma alijikuta akipewa kadi nyekundu kwa kosa la ‘kitoto’ la kumsukuma beki wa Gor Mahia.

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini