Wakenya watawala mbio za Berlin Marathon

Image captionWakenya Eliud Kipchoge na Gladys Cherono ndio mabingwa wa mwaka huu wa mashindano ya Berlin Marathon yaliyofanyika leo huko Ujerumani.
Wakenya Eliud Kipchoge na Gladys Cherono ndio mabingwa wa mwaka huu wa mashindano ya Berlin Marathon yaliyofanyika leo huko Ujerumani.
Kipchoge ambaye pia ni bingwa wa mwaka huu wa mbio za london marathon alikuwa anazuru mji wa Berlin kwa mara ya pili.
Kipchoge aliandikisha ushindi wa saa mbili dakika na sekunde moja.
Katika mashindano yake ya kwanza huko Berlin Kipchoge alimaliz katika nafasi ya pili nyuma ya bingwa Wilson Kipsang aliyeandikisha muda bora wa saa 2 dakika 03 na sekunde 23.
Kufuatia ushindi wake Kipchoge anakuwa mwanariadha wa 15 kutoka Kenya kushinda mbio hizo.
Mkenya mwengine Dennis Kimetto aliandikisha rekodi ya dunia ya saa 2:02:57 mwaka wa 2014.
Kwa upande wa wanawake Cherono alitangaza ujio wake katika jukwaa la riadha kwa kishindo alipoandikisha muda bora wa saa mbili dakika 19 na sekunde 25.
Hii ndio iliyokuwa shindano lake la pili tangu aanze kushiri mbio hizo za masafa marefu.
Cherono alisajili muda wa saa dakika 20 na sekunde tatu katika mashindano yake ya kwanza huko Dubai mapema mwezi januari.
Cherono sasa anakuwa ni mwanariadha wa tatu kutoka Kenya kutwaa taji hilo la Berlin.
Mkenya wa kwanza kuwahi kushinda huko Berlin alikuwa ni Tegla Loroupe (1999) alipoandikisha rekodi ya dunia ya saa 2: dakika 20:43.
Mwengine ni Florence Kiplagat (2011, 2013).

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …