Baada ya Kupoteza Mechi Nne, Kuna Dalili ya JKT Ruvu Kufanya Maamuzi Haya Magumu..
Ligi Kuu soka Tanzania bara imeendelea September 27 kwa mechi mbili kupigwa , huu ukiwa ni muendelezo wa mechi za round ya nne kwa timu za Ligi Kuu. Msimu wa Ligi 2015/2016 kila timu inaonekana kujiandaa na haitaki kupoteza mchezo wowote wa Ligi Kuu licha ya kuwa hali ni tofauti kwa klabu yaJKT Ruvu.
September 26 klabu ya JKT Ruvu ilishuka katika uwanja wa Karume ambao ndio uwanja wake wa nyumbani kwa msimu wa 2015/2016 kuikabili timu ya Stand United ya Shinyanga inayonolewa na kocha wa kifaransa aliyewahi kuifundishaSimba Patrick Liewing.
Fred Felix Minziro
Fred Felix Minziro
JKT Ruvu hawakuwa na matokeo mazuri katika mechi zao tatu za mwanzo kwani walipoteza zote kwa kufungwa na Maji Maji FC, Mbeya City, Yanga na September 26 walipoteza kwa mara ya nne mfululizo dhidi ya Stand United kwa goli 1-0.
Kufuatua matokeo hayo klabu ya JKT Ruvu imesafiri kuelekea Tabora kucheza mechi na Kagera Sugar bila kocha mkuu wa timu yao Fred Felix Minziro, hivyo kumezuka fununu huenda ikawa ametimuliwa kazi kocha huyo . Licha ya kuwa haijathibitika Minziro ameahidi ukweli kuweka wazi siku sio nyingi.