KIMENUKA! Mchungaji Peter Msigwa na Wenzake 61 wa CHADEMA Waswekwa Rumande!

Ramadhani--Mungi--november12-2014_0Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Ramadhani Mungi.
msigwaAliyekuwa Mbunge wa Iringa Mjini kwa tiketi ya Chadema, Mchungaji Peter Msigwa.
 
KAMANDA wa Polisi Mkoa wa Iringa, Ramadhani Mungi, amesema Jeshi hilo linamshikila aliyekuwa Mbunge wa Iringa Mjini kwa tiketi ya Chadema, Mchungaji Peter Msigwa na wenzake 61 kwa tuhuma za kufunga barabara ya Kihesa mjini Iringa.
Akizungumza kwenye kikao cha dharura na waandishi wa habari kwenye kijiji cha Migori kilichopo Jimbo la Isimani mkoani Iringa, RPC Mungi alisema Jeshi hilo lilimtia nguvuni Msigwa na wenzake hao jana Jumatatu majira ya jioni. 

Ilikuwa ni baada ya kupata taarifa kuwa watu hao walifunga barabara ya Kihesa wakiwazuia watu waliokuwa wakienda kwenye mkutano wa kampeni wa mgombea urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk John Pombe Magufuli uliokuwa ukifanyika katika viwanja vya Samora mkoani Iringa.
HABARI NA RICHARD BUKOS/GPL ALIYEKO IRINGA

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini