MAGUFULI: Watanzania Wamekata Tamaa!

John Magufuli, amesema amejipanga kulipa deni kwa Watanzania kwa kuleta mabadiliko ya kweli. Amesema pamoja na hali hiyo, anatambua namna wananchi walivyokata tamaa ikiwamo kushindwa kubadili maisha yao, kutokana na ubinafsi wa watu wachache ambao wameamua kujimilikisha rasilimali za nchi.
Ninajua Watanzania wanataka mabadiliko ambayo ni M4C yaani ‘Magufuli for Change’ na kwa lugha ya kawaida ni Magufuli kwa mabadiliko tena ya kweli,” alisema Dk. Magufuli. Akizungumza namna atakavyoubadili mji wa Iringa, alisema anajua changamoto zilizopo katika mkoa huo, ikiwamo kero ya barabara hasa za ndani. 
“Ninawashangaa watu wanasema eti CCM haijafanya kitu na wengine ni hapa hapa Iringa mjini tena mchungaji wa kondoo wa Mungu ambaye anazijua amri kumi za Mungu ikiwemo ya kutosema uongo. “Tena amekuwa akitukana ovyo ndani na nje ya Bunge nataka kuwaambia mawaziri nao ni binadamu wana nyongo…nataka kuwauliza ikiwa kila siku unamtukana waziri hivi kweli anaweza kukupa fedha za maendeleo, nichagueni mimi na wabunge wa CCM,” alisema.
Alisema anahitaji ushindi wa asilimia 99 ili wapinzani waisome namba kupitia masanduku ya kura.

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini