20 PICHAZ: Wataisoma Namba! Mambo ya IDD AZAN wa CCM Huko Kijitonyama Jijini Dar!

IDD AZZAN (1)
Mgombea ubunge iimbo la Kinondoni, Iddi Azzani akipokelewa na wakeleketwa wa Chama cha Mapinduzi (CCM), wakati akiingia kwenye Viwanja vya Shule ya Msingi Kijitonyama, tayari kwa kumwaga sera zake kwa wananchi wa kata hiyo.
IDD AZZAN (2)
Iddi Azzani akisalimiana na baadhi ya wanachama waliyojitokeza kumpokea muda mfupi baada ya kuwasili katika Viwanja vya Shule ya Kijitonyama alipokuwa akinadi sera zake kwa Wanakinondoni.IDD AZZAN (3)
Wakeleketwa wa chama hicho wakionyesha hali ya furaha wakati wa kumkaribisha mgombea ubunge wa Kinondoni katika kata ya Kijitonyama mapema jana.IDD AZZAN (4)
Mwenyekiti wa  CCM Kata ya Kijitonyama Shabani Japhary (kulia), akiongozana na Iddi Azzani wakati akiingia Viwanjani hapo.IDD AZZAN (5)
Iddi Azzani akiteta jambo na Shabani Japhary muda mfupi baada ya kupanda jukwaani kuelezea sera zake.IDD AZZAN (6)
Baadhi wakeleketwa wa chama hicho wakiburudika kwa muziki muda mfupi kabla ya mkutano wa mgombea huyo kuanza.IDD AZZAN (7)
Iddi Azzani akimtunza mmoja wa wapiga kura wake kabla ya mkutano huo kufunguliwa rasmi.IDD AZZAN (8)
Mgombea Udiwani kata ya Kijitonyama Frank Kamgisha (kulia), akiserebuka mmoja ya kikundi cha hamasa cha CCM kata ya Kijitonyama. IDD AZZAN (9)
Moja ya kundi la kudansi likitumbuiza kwenye kikao hicho. IDD AZZAN (10)
Mwenyekiti wa Vijana UVCCM kata ya Kijitonyama akisalimiana na mgombea wa ubunge wa kata hiyo Iddi Azzani.IDD AZZAN (11) Mgombea Ubunge jimbo la Kinondoni Iddi Azzani akiwa amebebwa juu kwa juu na baadhi ya wanachama wa kata ya Kijitonyama wakati akielekea kupanda jukwaani kwaajili ya kuongea na wananchi wa Kata hiyo.IDD AZZAN (12)
Iddi Azzani akinadi sera zake kwa wakazi wa Kata ya Kijitonyama.IDD AZZAN (13)
Iddi Azzani akimvisha kofia mmoja wa vijana waliyorudisha kadi ya Chadema na kujiunga rasmi na chama cha Mapinduzi mara baada ya kuhitimisha zoezi la kunadi sera zake.IDD AZZAN (14)
Mmoja wa wanachama wa CUF mwenye kanzu akionyesha kadi ya CCM muda mfupi baada ya kukabidhiwa na mgombea wa Ubunge wa chama hicho.
IDD AZZAN (15)
Iddi Azzani akiongea jambo na kijana huyo mara baada ya kuhamia CCM akitokea CHADEMA.IDD AZZAN (16) 
Iddi Azzani akinong'onezwa jambo na mmoja wa wapiga kura wake muda mfupi baada ya kuhitimisha kikao cha kumwaga sera zake.
HABARI/PICHA: MUSA MATEJA/GPL.

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini