Kisa cha Zaidi ya watu 60 wanaodhaniwa wafuasi wa Chadema kutiwa mbaroni hiki hapa


Polisi mkoani Iringa inawashikilia zaidi ya watu sitini wanaodaiwa kuwa wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kwa tuhuma za kuhatarisha amani kwenye barabara inayotoka katika uwanja wa michezo wa Samaro kwenda Kihesa.
Tukio hilo limetokea wakati Chama cha Mapinduzi CCM kupitia kwa mgombea wake wa Urais Dokta John Magufuli kufanya mkutano wa Kampeni za Urais kwenye uwanja wa michezo wa Samora Mjini Iringa.

Kadri siku zinavyojongea kufanyika kwa uchaguzi mkuu,hali ya kuanza kutokea kwa matukio yasiyo ya kawaida katika kampeni hizo yameanza kujitokeza.
Polisi ambao kisheri ndio wenye dhamana ya ya kulinda usalama wa raia na mali zao, imewatia nguvuni wafuasi 62 akiwemo mgombea ubunge kwa tiketi ya chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Mchungaji Peter Msingwa
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Iringa Kamishna Msaidizi wa Polisi Ramadhani Mungi amewaambia waandishi wa habari kuwa, kukamatwa kwa watuhumiwa hao inatokana na kupata taarifa za kiitelejensia kuwa kuna watu wamejipanga kufanya vitendo vinavyohatarisha amani
Kutokana na hali hiyo Polisi Mkoani Iringa imewanyooshea kidole wafuasi wa vyama vyote watakaokuwa chanzo cha vurugu na kuwataka kuacha kuvunja utulivu uliopo pamoja na kulinda amana ili kufanyika kwa uchaguzi uhuru na wa amani.

Wakati hayo yakijiri Mgombea Uraisi kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi CCM Dokta John Pombe Magufuli,ameendelea na kampeni kuomba ridhaa kwa wananchi wamchague awe raisi wa awamu ya tano.
Dokta Magufuli mwenye sifa ya kuwa mbali na ufisadi,anasema amejipanga kuhakikisha akiingia madarakani anatatua kero.Dokta Magufuli anasema kwake yeye ni kazi tu,asiyekubali kufanya kazi,ipo kazi

Dokta Magufuli na Ujumbe wake ameanza ziara ya Kampeni Mkoani Dodoma,ukiwa ni mkoa wake wa 18 tangu tume ya taifa ya uchaguzi iliporuhusu kufanyika kwa kampeni Agost 22.

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini