Je, Kweli Jeshi la Magereza TZ Limetangaza Ajira Mpya?! Jibu La Kamishna Lipo Hapa...

Katika siku za hivi karibuni, kumekuwepo na tangazo kuhusu nafasi za ajira katika Jeshi la Magereza linalodaiwa kuwa limetolewa na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza na kusambazwa kwenye baadhi ya Mitandao ya kijamii. Umma unajulishwa kuwa taarifa hizo siyo za kweli. 

Jeshi la Magereza linapenda kuufahamisha umma kuwa ajira hutolewa na kutangazwa kupitia Vyombo vya Habari pamoja na tovuti ya Jeshi la Magereza yawww.magereza.go.tz na si vinginevyo.
Hivyo, Jeshi la Magereza linawatahadharisha Wananchi wote kuwa macho na mitandao ya kitapeli inayotoa taarifa za kupotosha na kuleta usumbufu mkubwa kwani mfumo wa ajira ndani ya Jeshi la Magereza ni wa wazi na unafuata Kanuni na Taratibu za ajira za Utumishi wa Umma. 

Imetolewa na kusainiwa na, 
John C. Minja 
KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA 
29 Septemba, 2015

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini