MSIBA: KIGOGO WA CCM AFARIKI JIJINI DAR

Katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Ilala, Ernest Chale amefariki dunia katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam alipokuwa amelazwa kwa ajili ya matibabu.
Chanzo chetu cha kuaminika ndani ya CCM kililiambia Nipashe kuwa katibu huyo amefariki majira ya saa 5:30 asubuhi jana katika hospitali hiyo.
Alisema kuwa Jumatano ya wiki hii alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa shinikizo la damu na Alhamisi alipelekwa katika Hospitali ya Muhimbili na kulazwa wodi ya Mwaisela.

Alisema hali yake ilibadilika na hatimaye umauti ukampata.
Naye Katibu wa Siasa na Uenezi wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, Juma Simba Gadafi, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo.
Alisema Jumatano walikuwa wote kwenye kampeni na hali yake ilibadilika usiku akiwa usingizini.
CHANZO: NIPASHE

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini