MAAMBUKIZI KATIKA NJIA YA MKOJO (UTI)



Leo tutazungumzia tatizo la maambukizi katika njia ya mkojo Urinary Tract Infection (UTI) ugonjwa ambao unawasumbua sana wanawake wengi na watoto japokuwa hata wanaume huugua.

Maambukizi katika njia ya mkojo au kama unavyojulikana kwa wengi UTI huathiri mfumo wa mkojo ikiwa ni pamoja na Ureter ambayo ni kama bomba linalosafirisha mkojo kutoka kwenye figo, pia kibofu cha mkojo na mrija wa kutolea mkojo nje yaani Urethra.

Ugonjwa huu unaathiri zaidi kibofu cha mkojo na Urethra lakini unaweza pia kuathiri figo. Maambukizi haya yakiathiri sehemu za chini za kibofu cha mkojo kitaalam huitwa Simple Cystitis au Bladder Infection na maambukizi hayo yakitokea sehemu za juu za mfumo wa mkojo huitwa Pylonephritis au Kidney Infection.

Ugonjwa huu husababishwa na bakteria anayeitwa Escherichia Coli (E. Coli) na tatizo hili husababishwa kwa kiasi kikubwa na bakteria ambao makazi yao ya kawaida ni kwenye utumbo mpana, na hivyo huwa wanapatikana pia kwenye haja kubwa.Lakini baadhi ya watu wanaweza kupata tatizo hili kutokana na kuingiwa na fangasi ingawa pia zipo sababu nyingine chache.

Bakteria wa Escherichia Coli hawasababishi peke yao UTI bali huambatana na wengine waitwao Staphylococcus, Saprophyti cus, Pseudom onas, Enterobacter na kadhalika. Maambukizi katika njia ya mkojo lazima yawe ni kwenye njia ya mkojo na si pengine popote.

Wapo wanawake ambao wamekuwa wakidhani kwamba tatizo la kutokwa na uchafu ukeni ni ugonjwa huu, na hilo si sawa kwani huo ni ugonjwa tofauti kabisa na UTI.

Tunapozungumzia maambukizi katika njia ya mkojo, inamaanisha ni kutoka eneo la nje ya utupu hadi kwenye kibofu na kutoka kwenye kibofu hadi kwenye figo. Kama maambukizi yako katika eneo la kutoka kwenye kibofu hadi kwenye figo, kitaalam huitwa Lower Urinary Tract Infection na yakihusisha eneo la juu ya kibofu jina hubadilika na kuitwa, Upper Urinary Tract Infection.

SABABU ZA UTI KWA WANAWAKE

Mara nyingi maambukizi haya kwa wanawake husababishwa na kutojisafisha vizuri sehemu za siri na kuvaa nguo za ndani zilizochafu.Pia huweza kusababishwa na matumizi ya pedi za kike zenye kemikali ya kukata harufu ambazo huua bakteria wa asili wa eneo la uke na kuwapa fursa bakteria wanaosababisha maradhi kuzaliana kwa wingi.

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini