Nimepita kwenye Barabara za Mabasi ya Mwendokasi Dar, kabla hazijaanza kutumika tayari kuna uharibifu.. (Pichaz)
Ni good news kwamba kuzinduliwa kwa barabara za Mabasi ya Mwendokasi kabla haujaisha mwaka 2015, watu wa Dar ambao wamepata matumaini mapya kwamba ishu ya tabu ya usafiri kuingia katikati ya Jiji inaelekea kupatiwa ufumbuzi.
Lakini kingine ni kwamba kuna matatizo ya foleni kwenye Barabara zinazoingia katikati ya Jiji pia, hili nalo linaelekea kupatiwa utatuzi kabisa kwa sababu mabasi ya Mwendokasi yanapita kwenye Barabara zake pekeyake.
Ujenzi wa Barabara umekamilika kwa kiasi kikubwa sana na tunategemea Mabasi yaanze kazi ndani ya kipindi kifupi tu kuanzia sasa.. camera ya ripota wa millardayo.com imepita maeneo mbalimbali ambako tayari ujenzi ulikuwa umekamilika kwa kiasi kikubwa, na uharibifu umefanyika pia.