CCM YALAANI VIJANA 1500 KUJITANGAZA MASHOGA..SOMA HILI TAMKO LAO


Picha ya Maktaba
Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Mufindi Mkoani Iringa kimewataka vijana waliopo wilayani humo kuacha kujihusisha na masuala ya ushoga.


Akizungumza na waandishi wa habari jana,Katibu wa CCM Wilaya ya Mufindi,Jimson Mhagama alisema hatua ya vijana kuingia katika ushoga ni sawa na kulidhalilisha taifa.


Kauli ya Mhagama imekuja mara baada ya kuwepo kwa taarifa za vijana na wanafunzi 1500 wa elimu ya juu waliopo mkoani humo kujihusisha na vitendo vya ushoga, hali ambayo imeleta taswira mbaya.


Alisema ni vyema vijana hao wakaacha tabia hiyo na badala yake watafute pesa kwa njia halali na si kujiingiza kwenye maswala ambayo yanavunja heshima ya jamii na taifa kwa ujumla.


"Wanafunzi wa Elimu ya juu wanaojihusisha na ushoga wanadhalilisha vyuo vyao na familia zao, lakini CCM inapendekeza kuwa mwanafunzi atakayebainika kufanya mchezo huo afukuzwe chuo mara moja" Alisema Mhagama


Alisema umefika wakati kwa Bunge kutunga sheria kali na kuifanyia mabadiliko katiba ya mwaka 1977 kuweka kipengele kinachobana mambo ya ushoga.


Aliongeza,mtu akibainika ni shoga apewe adhabu kali ya kifungo cha miaka 30 jela

ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

Popular posts from this blog

Upepo wakwamisha Uokoaji Meli iliyozama

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini