Uwepo wa mabaka na madoa usoni ni tatizo linalowakabili watu wengi na kuwafanya kuhangaika huku na kule kutafuta dawa ili kukabiliana nalo, lakini hujikuta wakiishia kutumia vipodozi vyenye kemikali ambavyo huishia kuharibu ngozi za wengi wao. Zipo njia mbalimbali za asili, zinazoweza kukabiliana na tatizo hili ikiwamo matumizi ya papai.

 Wengi tumekuwa na fikra kuwa papai ni tunda linalofaa kuliwa na kutengenezwa juisi tu bila kufahamu kuwa lina matumizi makubwa zaidi ya hayo. Ukweli ni kwamba, licha ya papai kuwa ni tunda lenye umuhimu mkubwa katika mwili wa binadamu linapoliwa au kunywa juisi yake, pia linaweza kutumika kama dawa au kinga katika ngozi na kuifanya ionekane yenye mvuto wakati wote. 
Papai pia lina uwezo wa kuondoa madoa yanayowasumbua wengi katika ngozi hasa usoni na kuiacha ngozi iking’ara. Mchanganyiko wa papai na asali ni tiba nzuri kwa maradhi ya ngozi ukilinganishwa na matumizi ya vipodozi vingine vyenye kemikali. 

ya vipodozi vingine vyenye kemikali. Njia nyingine inayoweza kusaidia kuondoa mabaka na madoa mwilini ni majani ya alovera. Majani haya yanapaswa kupakwa na kusugua eneo liloloathirika, utomvu wake husaidia kufuta mabaka hayo. Jinsi ya kufanya Safisha uso kwa maji ya uvuguvugu kuondoa taka zote zilizopo, kisha kausha vizuri kwa kitambaa kikavu. 
Katakata papai katika vipande vidogovidogo, visage kwa kutumia mashine au twanga katika kinu mpaka vilainike kabisa na upate rojorojo. Changanya rojo uliyopata na asali, kisha endelea kukoroga hadi vichanganyike kabisa. Paka mchanganyiko huo usoni, kaa nao kwa muda wa dakika 15 hadi 20, kisha safisha uso.
 Kama utatumia alovera, fuata pia hatua hizi, huku ukisugua katika maeneo yote yaliyoathirika mwilini. Fanya hivyo mara mbili kwa siku kwa muda wa mwezi mmoja, utaona mabadiliko katika ngozi ya uso na madoa yote yatafutika.

ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

Popular posts from this blog

Upepo wakwamisha Uokoaji Meli iliyozama

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini