Mbarawa atoa siku tatu ukarabati wa reli



Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa amewataka watendaji wa Shirika la Reli nchini na Kampuni Hodhi ya Mali za Reli (RAHCO), kuhakikisha sehemu ya reli iliyosombwa na mafuriko wilayani Kilosa inaunganishwa ndani ya siku tatu. Profesa Mbarawa alitoa agizo hilo jana baada ya kukagua sehemu ya reli hiyo iliyosombwa na maji ya mvua kutoka Kilosa hadi Magulu ­ Kidete, kujionea athari .

“Fanyeni kazi usiku na mchana ili ikifika Alhamisi wiki hii, mawasiliano ya reli kati ya Mkoa wa Morogoro na Dodoma yawe yamerejea,” alisema Waziri huyo. Pia, aliwahakikishia wakazi wa vijiji vya Munisagara, Mkadage, Mzaganza, Magulu na Kidete wanaotumia usafiri huo, kushirikiana na mafundi wanaofanya ukarabati wa reli hiyo ili ukamilike kwa haraka. Profesa Mbarawa aliwataka pia wakazi waishio karibu na njia ya reli wilayani Kilosa,
 kupanda miti ili kuzuia mmomonyoko wa udongo unaosababisha mafuriko na kuifanya ibomoke kila mara. “Lindeni miundombinu ya reli na acheni uharibifu wa mazingira ili ujenzi wa mwaka huu uwe wa kudumu,” alisema. Naye Diwani wa Kidete, Mohamed Mbunda alimhakikishia Waziri Mbarawa kuwa wananchi wake watashirikiana na Serikali kulinda mazingira ili kudhibiti mafuriko yanayotokea kila mwaka. Mvua mafuriko hayo yameharibu reli umbali wa kilomita 315 kutoka Magulu­Kidete. Katika hatua nyingine;

 Waziri Mbarawa amewataka watendaji wa TRL na RAHCO kutafuta suluhisho la kudumu la madaraja 32 yaliyo katika mtandao wa Reli ya Kati ili yasiathiriwe na mafuriko ya mvua. “Fanyeni jitihada ili matatizo haya yasiwe yanajirudia mara kwa mara,” alisema Profesa Mbarawa.


ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

Popular posts from this blog

Upepo wakwamisha Uokoaji Meli iliyozama

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini