Mengine kutoka Hospitali ya Muhimbili kuhusu mashine za CT Scan..





Agizo la Rais Magufuli la kupatikana kwa mashine mpya ya CT Scan katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili limeonekana kuzaa matunda baada ya Serikali kununua mashine mpya ambayo imegharimu dola za Kimarekani milioni 1.7.

Kutokana na mashine ya awali kuharibika kila wakati Serikali imegharamia mashine mpya ambayo imeelezwa kuwa na uwezo mkubwa wa kufanya kazi tofauti na nyingine zilizowahi kutumiwa na hospitali hiyo.

Neema Mwangoko ambaye ni afisa Uhusiano wa hospitali hiyo amesema mashine hiyo mpya ina siku tatu tangu ifungwe na tayari imehudumia wagonjwa 26 mpaka sasa na bado ipo kwenye majaribio.

Naibu waziri wa afya Dk.Hamis Kigwangala ambaye alifanya ziara katika hospitali hiyo amepongeza hatua hiyo na kutaka watendaji waboreshe huduma zinazotolewa kwa wateja wake.

ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

Popular posts from this blog

Upepo wakwamisha Uokoaji Meli iliyozama

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini