SAD NEWS MEYA AUAWA SIKU MOJA BAADA YA KULA KIAPO


Meya wa Manispaa ya Temixco nchini Mexico aliyetajwa kwa jina la Gisela Mota Ocampo ameua kwa kupigwa risasi saa 24 baada ya kula kiapo na kukabidhiwa rasmi ofisi.
Duru kutoka nchini humo zimeeleza kuwa watu wenye silaha walivamia nyumbani kwake Jumamosi asubuhi (Januari 2, 2016) wakati familia yake ikiwa nyumbani hapo lakini walimuua yeye pekee.

Mwanasheria wa serikali wa Jimbo la Morelos alieleza waandishi wa habari kuwa katika tukio hilo, polisi walirushiana risasi na wavamizi hao na kufanikiwa kuwaua wawili kati yao. Alisema kuwa baadhi ya watu wazima na watoto wanashikiliwa na polisi wakihusishwa na tukio hilo na watafikishwa mahakamani.
Temixco inatajwa kuwa moja kati ya Manispaa zenye uhalifu wa jinai wa kiwango cha juu na maarufu kwa biashara haramu ya dawa za kulevya.

ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

Popular posts from this blog

Upepo wakwamisha Uokoaji Meli iliyozama

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini