Mwanamuziki Maarufu Auawa Baada ya Kupambana na Polisi na Kupigwa Risasi

Visa vya watu kuuawa vimekuwa vikiripotiwa mara kwa mara Bujumbura 
Mwanamziki mmoja kutoka Burundi amepatikana amefariki katika mji mkuu wa Burundi, Bujumbura baada ya kukamatwa na polisi, hii ni kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa kundi la wanahabari la SOS. 


Taarifa hizo zinasema kwamba mwili wa Pascal Tresor Nshimirimana ulipatikana Jumamosi eneo la Musaga, karibu na gereza kuu la Bujumbura. 


Polisi wanasema Pascal alijaribu kumnyang'anya bunduki afisa wa polisi, na akauawa na risasi ililofyatuka kutoka kwa bunduki hiyo kwa bahati mbaya.



Bw Nshimirimana alikuwa mmoja wa waandamanaji ambao walipinga muhula wa tatu wa Rais Pierre Nkurunziza 
Katika kisa kingine, mwili wa kiongozi wa vijana William Nimubona ulipatakana katika maeneo ya Kavuma jijini Bujumbura. 
Hata hivyo, hakuna taarifa huru za kudhibitisha mauaji ya kiongozi huyo.


Bw Nimubona alikuwa kiongozi wa mrengo wa vijana katika chama cha National Liberation Forces (NLF) kinachoongozwa na Agathon Rwasa, kiongozi wa upinzani aliyekubali kuchukua kiti cha naibu wa spika baada ya Rais Nkurunziza kushinda uchaguzi tata wa muhula wa tatu.

ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

Popular posts from this blog

Upepo wakwamisha Uokoaji Meli iliyozama

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini