Gigy, msanii Tekno ukweli waanikwa



Muuza nyago kwenye video za wasanii wa Bongo Fleva, Gift Stanford ‘Gigy Money’.

Mayasa Mariwata na Imelda Mtema
Siri imefichuka! Muuza nyago kwenye video za wasanii wa Bongo Fleva, Gift Stanford ‘Gigy Money’ ameibua gumzo baada ya ukweli kuanikwa kwamba alilala kwenye Hoteli ya Serena iliyopo Posta jijini Dar akijiachia na msanii kutoka Nigeria, Tekno Miles.

Kwa mujibu wa vyanzo vya kuaminika, usiku wa kuamkia Ijumaa, mrembo huyo alionekana akijiachia na jamaa huyo ambaye alitua Bongo kwa ajili ya kutumbuiza kwenye Ukumbi wa King Solomon uliopo Namanga jijini Dar.

‘Gigy Money’ akiwa na Tekno.

Kama hiyo haitoshi, ilidaiwa kwamba, katika kudhihirisha hilo, Gigy alitupia picha kadhaa kwenye mitandao ya kijamii akiwa na Tekno hivyo kupewa makavu laivu na mashabiki wakionesha kwamba kitendo hicho ni kujidhalilisha kwa kumshobokea staa huyo wa Ngoma ya Duro.

Kufuatia ishu hiyo, gazeti hili lilimsaka Gigy ili afunguke juu ya tukio hilo ambapo alikiri kukutana na kulala na jamaa huyo hotelini hapo.

“Wanaoponda waache waongee tu, mimi sirembi hata kidogo pale ninapotaka jambo langu litimie, ingekuwa nimegharamia kulipia hoteli sawa, lakini sijahusika hata kidogo na hilo, wamelipa wenyewe,” alisema.


ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

Popular posts from this blog

Upepo wakwamisha Uokoaji Meli iliyozama

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini