JKCI: Bado tunachunguza afya ya Pengo

Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) imesema bado inaendelea na uchunguzi wa afya ya Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Kardinali Pengo aliyelazwa hivi karibuni Hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Kauli hiyo ilitolewa jana na kaimu mkurugenzi wa JKCI, Profesa Mohamed Janabi wakati akizungumza na gazeti hili lililotaka kufahamu maendeleo ya kiongozi huyo. Profesa Janabi alisema baada ya kumtoa Chumba cha Uangalizi Maalumu (ICU) juzi na kumpeleka wodi ya kawaida, hali ya Kardinali Pengo inaendelea vyema. 

“Bado tunaendelea kumfanyia uchunguzi. Ikifika siku ya kumpa ruhusa ya kwenda nyumbani kwake tutampa. Ila kwa sasa tunaendelea kumpa matibabu ili hali yake iimarike zaidi,” alisema Profesa Janabi. Alhamisi wiki iliyopita, Kardinali Pengo anayekaribia kufikisha miaka 72, alilazwa hospitalini hapo baada ya hali yake kudaiwa kuwa mbaya. Januari Mosi, 
mwaka huu Rais John Magufuli akiwa ameambatana na mkewe Janeth walimtembelea kiongozi huyo wa kiroho na kufuatiwa na viongozi wengine wa kitaifa na wa dini. waliokwenda kumwona Kardinali Pengo juzi ni pamoja na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, Naibu Waziri wa Afya, Dk Hamis Kigwangalla na Waziri wa Nishati na Madini, 

Profesa Sospeter Muhongo aliyekwenda jana. Mwingine ni Askofu Msaidizi wa Jimbo la Dar es Salaam, Eusebius Nzigilwa ambaye aliwataka waumini wa Kanisa Katoliki Tanzania wazidi kumwombea Kardinali Pengo. Katibu wa Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Padri Aidan Mubezi alinukuliwa juzi akisema Kardinali Pengo akitoka hospitalini atazungumza vyombo vya habari juu ya afya yake. Oktoba15, mwaka 2014 wakati akihutubia kwenye ibada maalumu ya misa iliyoandaliwa na Utume wa Wanaume Katoliki (Uwaka), 
Jimbo la Dar es Salaam Pengo alizungumzia afya yake baada ya kutoonekana hadharani kwa muda mrefu kutokana na kuumwa. Hata hivyo, katika ibada hiyo hakutaja ugonjwa unaomsumbua.


ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

Popular posts from this blog

Upepo wakwamisha Uokoaji Meli iliyozama

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini