KUBENEA Linda Heshima yako katika Jamii... Sifurahishwa na Uhasama Uliopo na ZITTO KABWE

Watanzania tumekuwa na mila na desturi ya kupongezana pale tunapofanya vizuri na pia kukosoana tunapofanya vibaya. Ni kutokana na utamaduni huu nathubutu kukuandikia.

Awali ya yote mimi ni msomaji wa magazeti ya Mwanahalisi/Mawio ambayo wewe kama mmiliki au mwandishi wa habari unapitishia taarifa zako kwenda ktk jamii.

Nimeguswa kukuandikia baada ya kusoma matoleo ya magazeti yako mawili ukionyesha kuwa na vita baridi na Zitto Zuberi Kabwe.

Mimi kama msomaji ninayejinyima pesa yangu ili kununua gazeti lako hakika sifurahishwi saana kusoma uhasama uliopo kati yako na Zitto Kabwe.

Tumetoka ktk uchaguzi na kama Taifa tunahitaji kutoka hapa tulipo kwenda mbele zaidi. Hatuwezi kufikia malengo kama uhasama uliopo kati yako na Zitto unataka kutuambukiza sisi wasomaji kupitia gazeti lako, na wala hatuwezi kwenda mbele tukiwa na hulka tuliyotoka nayo huko nyuma.


Tambua nafasi uliyonayo ktk jamii kwa sasa ya Ubunge kwa maana ya mwakilishi wa wananchi hivyo unatakiwa tabia na matendo yako yafanane na nafasi muhimu uliyokabidhiwa na umma wa wana Ubungo.

Itaniwia vigumu sana kwangu mimi kuendelea kununua magazeti haya kama mtazamo wako kama kiongozi wa jamii hautabadilika. Kwa makala ya leo ktk gazeti lako la Mwanahalisi ukurasa wa 7 haina tofauti na magazeti ya mipasho ya Uwazi, Kiu na mengineyo.

Ni matumaini yangu kuwa kuchaguliwa kwako kuwa mbunge wananchi hawakukosea na hivyo unatakiwa kulionyesha Taifa kwamba hata ukiaminiwa kupewa nafasi ya juu unaweza tofauti unavyojionyesha kuwa wewe ni mtu wa visasi. ANZA MWAKA KWA KUSAMEHE BADILIKA.
-Jamii Forums


ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

Popular posts from this blog

Upepo wakwamisha Uokoaji Meli iliyozama

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini