Kagame kugombea muhula wa tatu, Marekani yalaani



Rais wa Rwanda, Paul Kagame amesema atawania muhula wa tatu wa Urais baada ya wananchi kupigia kura rasimu ya katiba inayomruhusu kufanya hivyo. Akihutubia taifa hilo siku ya mwaka mpya, Kagame alidai kuwa uamuzi wake huo umetokana na chaguo la wananchi wake. Wananchi wa Rwanda waliipigia kura rasimu ya katiba hiyo December 18 kumruhusu Kagame, 58, kuwania tena muhula mwingine wa urais mwaka 2017 wenye miaka saba. Katiba hiyo itamruhusu kuwania tena mihula mingine miwili ya miaka kumi hadi mwaka 2034. Hata hivyo Marekani imelaani vikali hatua hiyo.

ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

Popular posts from this blog

Upepo wakwamisha Uokoaji Meli iliyozama

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini