MAJONZI: Baada ya Kupotea Kwa Wiki Mbili, Staa wa Soka Ivory Coast Amekutwa Amefariki Mtoni Ujerumani

Ikiwa ndani ya wiki zisizo pungua tatu ulimwengu wa soka umepokea taarifa za vifo vya wanasoka wawili, mchezaji wa timu ya taifa ya Honduras Arnold Peralta na aliyekuwa mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya El Salvador Alfred Pacheco. January 2 ulimwengu wa soka umepokea taarifa za kifo cha beki wa zamani wa timu ya taifa ya Ivory Coast na klabu ya Wigan Athletic Steve Gohouri.

Steve Gohouri ambaye alikuwa mahiri katika nafasi ya beki amekutwa amefariki katika mto Rhine wa Ujerumani, taarifa ambazo zimetoka ikiwa alipotea kwa muda wa wiki mbili, pasipo kujulikana wapi alipo, wiki mbili zilizopita aliripotiwa kupotea na kutafutawa bila mafanikio hadi January 2 mwili wake ulipokutwa mto Rhine. 
Mto Rhine


Staa huyo ambaye amefariki akiwa na umri wa miaka 34, aliwahi kuichezea klabu ya Wigan Athletic ya Uingereza kuanzia mwaka 2010 hadi mwaka 2012, lakini amechezea timu yake ya taifa ya Ivory Coast toka mwaka 2006 hadi mwaka 2011 ndio alianza kukosekana timu ya taifa. 
ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

Popular posts from this blog

Upepo wakwamisha Uokoaji Meli iliyozama

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini