Professor J kuihamishia studio yake Mikumi

ProfessorJay&JcB
Msanii mkongwe wa Hip Hop na Mbunge wa Jimbo la Mikumi, Joseph Haule ‘Professor Jay’, amesema ana mpango wa kuihamishia studio ya Mwanalizombe kwenye jimbo lake ili aweze kutekeleza ahadi ya kuinua sanaa. 
Akizungumza na gazeti la Mtanzania Jumatatu hii, Professor Jay alisema moja ya ahadi alizowaahidi wakazi wa Mikumi kwenye kampeni zake ni kuibua vipaji vipya. “Mikumi kuna vipaji vingi vya muziki lakini hakuna aliyeweza kuviibua kwa miaka mingi, ila mimi nikiwa kama Mbunge wao nitatekeleza ahadi hii kwa kuihamishia studio yangu Mikumi ili wasanii chipukizi waweze kufanya kazi zao,” alisema Profesa Jay. 
Mwanalizombe ni studio inayomilikiwa na msanii huyo ipo maeneo ya Mbezi Luis, jijini Dar es salaam na imeshatoa nyimbo kali kama Makamanda wimbo wa Sugu, Tatu Chafu na Kipi Sijasikia chini ya mtayarishaji Villy. 


ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

Popular posts from this blog

Upepo wakwamisha Uokoaji Meli iliyozama

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini