ELEWA UNDANI WA UGONJWA WA KIFUA KIKUU (TB)-2
Naendelea kuelezea undani wa ugonjwa wa kifua kikuu ambapo leo nitazitaja dalili zake. Dalili za kifua kikuu hutegemea sana ni mahali gani bakteria wa TB wanakuaw. Kwa kawaida bakteria wa kifua kikuu wanakuwa kwenye mapafu na kusababisha kifua kikuu cha mapafu. Kifua kikuu cha mapafu kinaweza kusababisha kifua kikali kinachochukua zaidi ya wiki tatu, maumivu ya kifuani na kukohoa damu au makohozi. Dalili nyingine za ugonjwa wa TB ni pamoja na udhaifu au uchovu, kupungua uzito, kukosa hamu ya kula, baridi, homa na kutoka jasho usiku. Kifua kikuu tuli hakina dalili. TIBA Kwa kawaida, mgonjwa wa kifua kikuu anatumia vidonge kila siku wakati wa matibabu yanayosimamiwa. Ugonjwa wa kifua kikuu kikali unaweza kutibiwa kwa mchanganyiko wa antibiotics. Mchanganyiko sahihi wa dawa za kifua kikuu hutoa kinga na tiba. Tiba inayofaa humwezesha haraka mgonjwa wa kifua kikuu kutoambukiza na kwa hiyo huzuia kuenea zaidi kwa kifua kikuu. Kufanikisha tiba ya ...