Mgombea Ubunge KINGWENDU Ataja Vipaumbele Vyake Akiingia Mjengoni!

Msanii wa filamu za vichekesho, Kingwendu ambaye mwaka huu anawania ubunge katika jimbo la Kisarawe, amesema akifanikiwa kuingia bungeni atawatumikia wananchi wa Kisarawe na kwamba atapumzika kufanya filamu kwa miaka mitano.
Kingwendu.._full
Kingwendu amesema anafuata sheria ya kukubali kuwatumikia wananchi na sio kufanya shughuli nyingine tofauti.
“Kazi kubwa nitaifanya kwaajili ya watu wangu walionichagua,” amesema.
“Maji, barabara pamoja na afya ni vipaumbele vyangu. Lakini kwa upande wa sanaa nitahakikisha msanii anapata haki yake katika kazi anayoifanya. Tutapambana na wezi wanaotuibia kazi zetu. Ingawa nitapumzika kufanya kazi za sanaa kwa miaka yote nitakayokuwa bungeni, lakini nitakuwa pamoja na wasanii katika harakati mbalimbali za maendeleo.”

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini