USAJILI ULAYA: Kevin De Bruyne kavunja rekodi ya Raheem Sterling Manchester City (Picha)

Klabu ya Manchester City ya Uingereza ambayo ilikuwa ni moja kati ya vilabu vingi vilivyo kuwa vikihusishwa na kumsajili kiungo mshambuliaji wa kimataifa wa Ubelgiji na klabu ya Vfl Wolfsburg ya Ujerumani Kevin De Bruyne, August 30 imetangaza kumsajili rasmi.
Kevin-De-Bruyne-signs-for-Manchester-City
De Bruyne ambaye ana umri wa miaka 24 alisajiliwa muda mchache baada ya kufanyiwa vipimo vya afya, amejiunga katika klabu hiyo kwa mkataba wa miaka sita, Kuwasili Etihad kwa Kevin De Bruyne kunaweka rekodi mpya ya klabu hiyo kwani ndio atakuwa mchezaji wa gharama zaidi katika klabu hiyo.
PAY-Kevin-De-Bruyne-signs-for-Manchester-City (1)
De Bruyne amejiunga na Man City kwa ada ya uhamisho wa pound milioni 54 na kuvunja rekodi ya usajili wa klabu hiyo kwani kabla ya kuwasili klabuni hapo,Raheem Sterling ndio alikuwa mchezaji aliyesajiliwa kwa pesa nyingi zaidi, dau la pound milioni 49 lilitosha kumtoa Liverpool na kumleta Etihad.
Kevin-De-Bruyn-on-his-way-to-Manchester-from-Germany
Uhamisho wa kiungo huyo wa kibelgiji bado unakuwa haujavunja rekodi ya usajili ya wachezaji Uingereza kwani hadi sasa Man United ndio klabu pekee ambayo bado inashikilia rekodi ya usajili kwa dau kubwa baada ya kutumia pound milioni 59.7 kumleta Angel di Maria akitokea Real Madrid ya Hispania msimu uliopita.

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini