NJEMBA Yafanyiwa KITU MBAYA Mbele ya Mkewe!

IMG_0109Akiminyiwa kichapo.
 Richard Bukos
 Hii kali! Njemba mmoja ambaye jina halikupatikana amekula kipigo mbele ya mkewe ambaye alifanikiwa kukimbia baada ya kudaiwa kufanya jaribio la kuingia kwenye onesho la Bendi ya FM Academia ‘Wazee wa Ngwasuma’ kwa kutumia tiketi feki, Ijumaa lina kisa na mkasa. 

Tukio hilo lililoshuhudiwa na mwanahabari wetu lilijiri mwishoni mwa wiki iliyopita kwenye Ukumbi wa Club East 24 iliyopo Mikocheni jijini Dar ambapo jamaa huyo alifika kwa Bajaj, akiwa na mrembo matata aliyetinga viatu virefu vya mchongoko na kigauni kifupi.
IMG_0124Wawili hao walishuhudiwa wakisogelea getini kwa mikogo huku wakiwa wameshikana viuno ambapo nuksi ilianzia pale walipowafikia wasimamizi wa getini na kuwaonesha tiketi.
 Katika hali ya kushangaza, ghafla jamaa huyo alishtukia akilambwa kofi la uso na baunsa wa Kampuni ya Black Ninja aliyefahamika kwa jina moja la Hamidu na kuanza kuhojiwa alikoipata tiketi hiyo. 

Wakati akijiandaa kujibu, yule mwanamke aliyekuwa naye ambaye alidai ni mkewe alipoona kimeanza kunuka kabla hajaionesha tiketi yake alianza kurudi nyuma akinyata kisha akajichanganya kwenye magari yaliyopaki nje na kutoweka. 

Baada ya kula kichapo ‘hevi’, njemba huyo alikuwa akiwataja watu hovyo kuwa ndiyo waliomuuzia tiketi hiyo, kwanza alimtaja rasta fulani ambaye ni mmoja kati ya mabaunsa hao kisha akabadilika na kumtaja mtu mwingine na kuwachanganya waliokuwa wakimhoji.
Kufuatia kauli zake kupishana walimtaiti na kumpeleka polisi.

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini