Kama Kipimo Cha Ushindi ni Idadi ya Watu, LOWASSA Ndiye Rais! CCM Chali, Imeshindwa Vibaya!

Wanabodi,
Nimepita hapa Jangwani kwenye uzinduzi wa kampeni za UKAWA, mchana wa Jumamosi tarehe 29/8 saa 8:45, kitu nilichokishuhudia, Kama Kipimo Cha Ushindi ni Idadi ya Watu, then, Lowassa Ndiye Rais Wetu!. Kwa upande huu wa idadi ya watu wa leo, nikilinganisha na idadi ya watu siku ya ufunguzi wa Mkutano wa CCM, then, CCM imepigwa chini, imeangushwa Chali!, Imeshindwa Vibaya!.

Hii inamaanisha, kama umati huu wote wamejiandikisha, na wote watajitokeza kupiga kura hiyo siku ya uchaguzi, hata CCM waibe vipi kura, kwa kuitumia NEC, kura hazitatosha, mshindi wa uchaguzi huu bado atakuwa ni Edward Lowassa!.

Lakini kama ni kweli, hawa wenye boda boda, bajaj na umati uliojitokeza wamehongwa pesa ili kuleta tuu ujazo wa wingi wa watu, lakini hawajajiandikisha kupiga kura na sii wapiga kura, then hakuna ubishi, mshindi ataendelea kuwa ni CCM!

Pasco wa jf, sio mwanachama, mfuasi au mshabiki wa chama chochote cha siasa, au mgombea yoyote, bali ni mkereketwa wa demokrasia ya kweli ndani ya bunge, ambaye anaamini kwenye ukweli na uwazi!.
Pasco, JF.

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini