CCM Yazidi Kujikaanga Yenyewe Kuhusu LOWASSA

Akihutubia mkutano wa (NEC) ya CCM Lowasa alinukuliwa akieleza hatua kwa hatua namna kampuni ya kitapeli ya Richmond ilivyopewa zabuni ya kufua umeme wa dharura nchi ni na kwamba Rais Kikwete anahusikamoja kwa moja kwenye mkataba huo.

Akiliambia kikao cha NEC mjini dodoma "Hakuna jambo nililolifanya ambao wewe Rais Kikwete hukulifahamu au hukunituma" kuhusu Richmond/Dowans. "Alisema mwenyekiti natukwanwa kwa ufisadi wa Richmond? Sasa kosa langu ni lipi?

Ni kule kukubali kuwajibika kwa ajili ya serikali yangu na chama chetu? Kwanini nihukumiwe kwa kisa hilo?" Huku akimtolea macho kikwete Lowassa alisema, "Unakumbuka vyema jinsi nilivyotaka kuvunja mkataba ule. Nilikupigia simu ukiwa nje ya nchi,lakini ulisema umepata ushauri wa kamati ya makatibu wakuu, ushauri ambao ulisababisha mkataba usivunjwe??"

Lowasa alisema Kikwete anafahamu kila kitu kwa kua ni yeye aliyeridhia kampuni ya Dowans Holding corporation SA, kupewa kazi hiyo baada ya Richmond kushindwa kuleta umeme. Katika muda wote ambao Lowassa alikua akizungumza ndani ya NEC Samwel Sitta alikua kimya kwa hofu kuwa Lowassa ataweza kumuumbua kwa kufichua zaidi yaliyofichwa juu ya alivyotumika kwa maslahi BINAFSI.

Mara kazaa Rais kikwete aliyekua akiendesha kikao hicho alimuangalia Sitta kama ishara ya kumzuia kuzungumza, jambo ambalo lilitibitisha maelezo ya Lowassa hausiki na sakata hilo.

Naye Mr Ben naye aliyekuapo mkutanoni humo alimshawishi Rais kikwete kutowapa nafasi watu wengine baada ya Lowassa kuzungumza. Kwa CCM nafikiri huu ungekua wakati muafaka wa kumwajibisha bwa ENL lakini mambo yamekua magumu kwao na kiutendaji wameshindwa kufanya hivyo japo walitumia juhudi kubwa kumchafua kupitia viongozi vibaraka wa ndani ya chama waliokua ndani ya payroll ya chama hicho.

Lakini mpango wa kuwatumia baazi ya kumchafua kati ya wajumbe 32 ni kuzidi kupoteza dira zaidi na zaidi licha ya chama kuonekana wazi kimepoteza muelekeo kwa kauli za kiuchochezi na za kufikirika za viongozi wao "tayar CCM imeshalikomboa taifa hili na kwamba wanaosema wanataka kulikomboa ni wapumbavu na malofa" japo mkapa na wenzake wanajua kuwa wanazungumzia ukombozi mpya,hawazungumzii BENDERA. Wanazungumzia Uhuru kamili wa kushika uchumi na utu wa MTANZANIA. Wanazidi kujikaanga kimipango na kwakauli zao wenyewe.

Rais kikwete alisikika akisema kwa kejeli mbele ya vyombo vya habari kua picha zinazomfata mafuriko Lowassa ni za kuunga ungu tu na wala sio halisi...akiwa wameshindwa kudhiirisha hilo japo kwa kutaja chango flani kinachohusishwa kwa kujiusisha na upotoshaji wa namna hiyo na kuthibitisha wanasimamia kucha.
Naomba niwasilishe karibuni wanjanvi tujadili.
Source: Jamii Forums via wazohuru

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini