NI VIDOGO SANA LAKINI VINAWEZA KULINOGESHA PENZI LENU!

Mpenzi msomaji wangu, leo nikupe siri kubwa ambayo huifahamu na huenda unatafuta dawa ya kulienzi penzi lako au kulinogesha ili mpenzi wako adumu na wewe.Nikueleze ukweli tu kwamba, hakuna dawa ya mapenzi katika ulimwengu huu, dawa ni wewe mwenyewe hasa ukiamua kufuata misingi ya mapenzi.
Inawezekana unajua ila unadharau au hujui kabisa sasa leo nitakuambia dawa yenyewe ni nini.Hivi hujawahi kuona kitu ukikiangalia wewe mwenyewe unakiona hakina maana au unakiona ni kidogo lakini ukamfanyia mpenzi wako ndiyo unakuwa umemroga kabisa na kumfanya akuhitaji na kutamani kuwa na wewe wakati wote?Miongoni mwa vitu ambavyo ni vidogo lakini ni vikubwa kwa wapenzi wetu hasa wa kike ni pamoja na hivi vifuatavyo.

Kumpikia 
Mwanamke ukimpikia chakula kuanzia kukiandaa mpaka yeye akakila hii huwa ni sumu kubwa ambayo humfanya ajione amefika. Siyo rahisi akaenda kwa mwingine eti kwa kufuata pesa ama gari kwani mwanamke ni mtu wa kuridhika kwa vitu vidogo wakati mwingine.Nakwambia mpenzi msomaji wangu kwa sababu nimewasoma wanawake wengi wanapenda mwanaume anayejali na mara nyingi kupikiwa huwa ni kitu adimu.

Wengi wetu tunajua hasa kwa mila za Kiafrika mwanamke ndiye huwajibika jikoni kwa kumuandalia mwanaume, ni wachache ambao huamua kumpikia mwanamke.Kutokana na uafrika wetu imefikia hatua ya watu kumuona mwanaume anayempikia mwanamke kuwa amepewa limbwata kwa sababu si kawaida, wanasahau kuwa kufanya hivyo ni kuongeza upendo kwa mwanamke.
Kumlisha chakula 
Hii ni dawa nyingine ambayo ukimfanyia mwanamke hujikuta anakumisi hata uwapo mbali.
Wanawake wengi ni wavivu wa kula au utakuta akila kidogo anaacha. Ili kuongeza mapenzi hebu jaribu kumlisha uone jinsi atakavyokula na wewe mpaka mwisho.Kitendo cha wewe kumlisha huwa kinamfanya ajihisi anapendwa sana kama mtoto na humpa nafasi ya kukudekea.

Utani 
Watu wengi hujiuliza hivi f’lani alimpendea nini f’lani wakati hana kitu. Siyo kitu kwa wakati mwingine nilichojifunza wanawake wengi hupenda mwanaume ambaye anaweza kumfanya akacheka na kupoteza ‘stress’ alizonazo.
Mwanamke ukimpa nafasi ya kumtania au kumfanyia utani utakaoamsha kicheko huwa anakukumbuka wakati wote na kama ni mpenzi wake hutamani kuwa na wewe wakati wote.

Vizawadi 
Vizawadi vidogo vidogo kama pipi, apple, chokleti, keki siyo kwa watoto tu hata watu wazima. Ukimpelekea mkeo zawadi kama hizo anathamini na kuona umempa kitu kikubwa kuliko unavyodhani.
Wanawake hawatofautiani sana na watoto, nao hupenda kuoneshwa mapenzi kwa njia hii.
Kwa hivyo nilivyokuandikia hapo hakika ni vitu vidogo lakini ukimfanyia mkeo au mpenzi wako utaona jinsi penzi lenu litakavyochanua.

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini