SHTUKA! Haya ni mambo ambayo watu waliofanikiwa hawawezi kukuambia kazini!

Huwezi kujenga mtandao imara wa kitaaluma kama hauko wazi kwa wanataaluma wenzako lakini unatakiwa kufanya hivyo kwa umakini mkubwa. Katika suala la kuwa muwazi inabidi kukumbuka kuwa vitu vingine ukiwa muwazi vinaleta madhara kwenye taaluma yako na kazi yako pia;
Unapoongelea maisha yako kwa ujumla inakubidi uwake sanaa ya kimaongezi. Kama kuna kitu ambacho unajua au una wasiwasi kinaweza kuathiri mahusiano yako na kazi inakubidi ubaki nacho mwenyewe ili kisije kukuletea shida hapo baadaye.

Yafuatayo ni mambo ambayo watu waliofanikiwa huwa hawayasemi na wewe hutakiwi kuyasema ili kujilinda mwenyewe na taaluma yako.

1. Watu wengi huwa hawasemi kuwa hawaipendi kazi hiyo wanayoifanya

Kitu cha mwisho kabisa ambacho watu hutaka kukisikia katika kazi ni namna gani mtu anavyolalamika kuhusu kazi yenyewe. Ukifanya hivyo tayari unaingia katika watu ambao huwekewa matatizo makubwa na wakubwa wao wa kazi na kuonekana hawapo pamoja nao. Watu wakisikia habari kuwa hupendi hiyo kazi unawavunja moyo hata kama utakuwa unafanya nao kazi. Hawatakuamini hivyo watakutafutia mtu wa kuchukua nafasi yako.

2. Watu wengi hawawezi kusema kwamba mmoja wao hana uwezo wa kazi

Kila sehemu ya kazi lazima kuna watu ambao hawana uwezo wa kazi na uwezekano huo upo kwamba kila mtu anajua wewe hauna uwezo wa kazi ila wameamua kunyamaza. Kwa mabosi wengi kama hana uwezo wa kukusaidia kuboresha uwezo wako njia mbadala ni kukufukuza kazi kwakuwa hakuna kitu anachopata kama akikutangazia kuwa wewe si mtendaji wa kazi. Na unapotokea kwamba unapakaza kuwa mwenzako hana uwezo wa kazi hiyo ni fikra ya kutoka uonekane kama wewe ni bora kuliko mwingine. Unaweza kufanya hivyo kuongelea watu wengine kwa watu wengine kumbuka kuwa na wengine wataendelea kuongea juu yako.

3. Watu wengi hawapendi kusema wanapata mshahara kiasi gani

Wazazi wako wangependa kujua unapata kiasi gani na hata mke wako labda na hata watoto wako, lakini kazini hicho kitu ni kigumu na wala hakitakiwi kuzungumzwa kabisa kwani kitaleta matokeo mabaya. Ni ngumu sana kuwapatia watu mishahara kwa usawa, itakapojulikana unapata kiasi gani watu wanaanza kupima na kazi ambazo unazifanya kama zinaendana na mshahara unaopata. Vile vile watu wanapojua mshahara wako wataanza kupima kila kitu kulingana na mshahara unaopata, na inawezekana kama wewe ndio bosi wao ikaleta mzozo wa chini chini.

4. Watu wengi hawawezi kuongelea misimamo yao kisiasa na kidini

Watu katika siasa na imani zao zimejengeka kwa ukaribu kiasi kwamba wanajikuta ndio utambulisho wao hata kazini. Watu waliofanikiwa hasa na kutambua maisha, taaluma, siasa na Imani wanachukulia mambo hayo kwa umakini mkubwa. Kwasababu moja ni rahisi kuingia kwenye mzozo katika kazi kwasababu ya mambo hayo ya kisiasa na kiimani endapo ukaendelea kuyaongelea hasa kazini.

Kinachotokea ni kwamba kushindwa kuelewana au kutofautiana kwenye jambo la kisiasa na kidini inaweza ikaonekana kwamba umemtukana mtu au hukumtendea haki kutokana na kile anachokiamini au upande wa kisiasa ambao yuko.

Na hiyo inaleta mtafaruku katika kazi na kuzua ugomvi mkubwa na hii ina ushahidi mkubwa maeneo mengi sana. Kama unataka kufanikiwa unatakiwa kutofautisha kazi , siasa na imani. Huwezi kujua wengine wanaamini nini na wako tayari kuingia kwenye mzozo mkubwa kwa ajili ya mambo hayo. Ukiweza kuonekana haufungamani na upande wowote hiyo ni nzuri kwako kwani lolote linapotokea, unakuwa kwenye ukanda wa amani na kuheshimika.

Hii ina maanisha unaweza kusikiliza watu na mitazamo yao ya kisiasa na kiimani na kuweza kujibu kwa hekima ambayo haitaleta ugomvi au kutokuelewana kiasi kwamba ukaathiri hali ya hewa kazi hapo.

5. Watu wengi huwa hawasemi wanachokifanya kwenye mitandao ya kijamii

Kitu cha mwisho ambacho bosi wako anataka kukiona anapoingia kwenye mitandao ya kijamii kuhusu wewe ni picha mbaya. Unapokuwa na picha mbaya au lugha chafu kwenye mitandao unajishushia heshima yako na hata mtazamo ambao ulikuwa unatazamwa nao unabadilika.
Watu ambao wanajua vizuri athari zake kitaaluma huwa hawafanyi hivyo, kwani kama haitakuathiri leo basi kesho utaathirika tu. Hii inamaanisha matatizo na mambo yako unatakiwa ukae nayo wewe tu usiiweke kwenye mitandao kwani ni rahisi mtu kutumia kinyume na matakwa yao.

6. Hawaongelei vitu vya vyumbani mwao

Kama mambo yako ya ndoa ni mazuri au si mazuri hiyo ni habari ambayo huwezi kuielezea kwenye eneo lako la kazi. Ukifanya hivyo unajijengea picha mbaya kabisa. Vile vile hutakiwi kuongelea mtu yeyote anachofanya chumbani kwake hata kama unajua au uliambiwa kwa namna yoyote ile. Wewe ndiye utaonekana una matatizo na watu hawatakuangalia kama walivyokuwa wanakuangalia kwa heshima.

7. Huwa hawasemi kama wanahitaji cheo/kazi ya mtu fulani

Unapoelezea dira na malengo yako kazini ni rahisi kuingia kwenye mtafaruku na watu mbalimbali kutokana na ubinafsi au kutofautiana katika shirika au kampuni hiyo. Wafanyakazi bora hupenda timu nzima ifanikiwe na si wao peke yao. Haijalishi una malengo gani utaharibu pale tu ukielezea mambo yako binafsi au ubinafsi wako.

8. Jinsi walivyokuwa wakifanya mambo ya ajabu chuoni na shuleni

Mambo yako ambayo ulifanya zamani yanasema vitu vingi sana kuhusu wewe mwenyewe. Kama ulifanya kitu cha kijinga miaka 20 iliyopita itasababisha watu wakutafsiri tofauti na kabla vile ambavyo walikutafsiri kabla ya kuwaambia. Mambo mengine watu hawapaswi kujua ulikuaje hapo kabla na mambo mengine watu wanapaswa kujua na hayana madhara kwenye taaluma yako.

9. Kuwa wanakunywa na kufanya starehe kiasi gani mwisho wa wiki

Kutokana na kutokujua watu huwa ni wawazi jinsi gani walivyofanya mambo fulani wakati wa siku za mwisho wa wiki. Kama wewe ni mfanyakazi bora ni mfanyakazi bora wakati wote? Hapana haiko hivyo. Unapoongelea jinsi ulivyokunywa sana si kwamba watu watakuchukulia kwamba una maisha yenye uchangamfu na furaha, hapana wengine watakuona ni mlevi fulani hivi.

Kitu hicho hicho wataanza kuona haueleweki wala hautabiriki, hujakomaa kifikra na hauna maamuzi yenye tija. Watu wengi huwadharau watu ambao wanatumia pombe au vitu vingine vya kulevya na kama wewe unachukulia sifa kuviongelea kazini haujui una haribu kiasi gani heshima yako.

10. Huwa hawafanyi utani wa kukera

Kama utakuwa makini na kujifunza kutoka kwa watu wengine inakubidi uwe makini na aina ya maneno yanayotoka mdomoni kwako. Kuna watu ukiwatania na maneno fulani au juu ya vitu fulani wanakerwa sana na utani huo.

11. Huwa hawasemi kama wanatafuta kazi nyingine

Kuna mtu mmoja alisema alipokuwa mtoto alimwambia kocha wake kwamba ataachana na timu aliyokuwa akiichezea kwa wiki mbili zijazo. Anasema, “katika zile wiki mbili nilisugua benchi kwa muda wote na wakati mwingine watoto wenzangu walikuwa hawataki kukaa na mimi, nilikuwa najisikia vibaya sana. Nikagundua ya kuwa nilikurupuka na kufanya maamuzi ambayo sikutakiwa kuyafanya.” Hivyo unapokuwa kazini unatakiwa kutunza mambo yako kwani mara tu mabosi wako watagundua uko katika mpango wa kutafuta kazi nyingine wanakuweka kando na utajikuta wanaachfa chukka majukumu kabisa.

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini