Alama za MAGUFULI Zawatia JEURI Zaidi CCM



CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimeendelea kujivunia kukubalika kwa mgombea wake wa urais, Dk John Magufuli, kutokana na kazi alizofanya kuonekana katika kila mkoa na kila wilaya.

Mjumbe wa Kamati Kuu (CC) ya Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, William Lukuvi alisema jana katika Jimbo jipya la Madaba kwamba, hakuna mkoa wala wilaya ambayo mgombea huyo hajafanya kazi.


Lukuvi alisema hakuna mahali ambako Dk Magufuli hajasimamia ujenzi wa barabara zinazorahisisha mawasiliano na usafirishaji, ambao ni muundombinu muhimu katika kuboresha maisha ya Watanzania kiuchumi, kisiasa na kijamii.
“Huyu (Dk Magufuli), mmemuona na kazi alizofanya mnazijua, sasa wale wengine (Ukawa), si mmewaona wamezindua kampeni zao…sasa wakija mna haki ya kuwasikiliza, lakini muwe makini wasiwauzie mbuzi kwenye gunia, waambieni wamwage sera,” alisema Lukuvi.


Akizungumza na wananchi wa jimbo hilo, ambalo zamani lilikuwa sehemu ya Jimbo la Peramiho, kabla ya kugawa Ilani ya CCM kwa wagombea wa ubunge na udiwani, Dk Magufuli alisema hao wengine ( kundi la Umoja wa Katiba ya Wananchi, Ukawa), hawana ilani, kwa kuwa kila chama kina ilani yake.
-Habari leo

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini