Je, Ni kweli HUSSEIN BASHE Anamuunga Mkono LOWASSA?! Yeye Mwenyewe Afunguka Kihivi...

Baada ya habari hiyo hapo juu kusambaa sana kwenye mitandao ya kijamiii Hussein Bashe amekanusha habari na kusema ni uzushi kwa sababu mpaka muda huu hajazindua kampeni kwenye jimbo lake la NZEGA mjini. Ikumbukwe Bw. Bashe alikuwa ni mfuasi mkubwa sana wa Mhe Lowassa na huwezi kutaja harakati za kisiasa za mhe Lowassa bila kutaja jina Bashe!

Bw Bashe alikuwa ni mtetezi mkubwa sana Lowassa akiwa CCM kwa sababu alikuwa na uwezo kuwakosoa na wakina Nape bila kuogopa kwa hiyo watu wengi walitegemea kuwa angehama na Lowassa kuja UKAWA lakini haikuwa hivyo lakini yeye mwenyewe amesema ana maamuzi yake binafsi ndio maana ameendelea kubaki CCM.

KAULI YA HUSSEIN BASHE KUPITIA UKURASA WAKE WA FACEBOOK
Mimi Hussein Mohamed Bashe napenda kukanusha taarifa zilizozagaa kwenye mitandao ya kijamii kwamba si za kweli na ni zakutunga.
Binafsi bado zijazindua kampeni yangu rasmi. Naomba Watanzania wapuuzie huo uongo.

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini