Uzinduzi wa kampeni CHADEMA, Magufuli na ‘People’s Power’?, Slaa Kuibuka kesho? Sumaye + Kipindupindu Pwani je!? (Audio).

trending-news
Uchambuzi wa magazeti kupitia @CloudsFM umefanyika tayari, ninazo zile zote zinazoweka headlines kwenye magazeti leo 28 August 2015 baadhi zikiwa… 

Hatimaye CHADEMA waruhusiwa kutumia viwanja vya Jangwani kuzindua kampeni zake kesho… Edward Lowassa asema jambo la madiliko kwenye Taifa hili ni lazima akipata ushirikiano kutoka kwa wanawake. 

Mgombea Urais kupitia CCM John Magufuli asema ‘Peoples Power’ wampe kura zao ili afanye kazi… Wilbroad Slaa kuibuka kwenye uzinduzi wa kampeni za CHADEMA kesho?… Frederick Sumaye atarajia kutangaza Chama atakachojiunga.
NEC imetoa ufafanuzi kuhusu mashine za uandikishaji BVR wasema baada ya Uchaguzi Mkuu mwezi October mashine hizo zitaenda NIDA… Lawrence Masha anyimwa dhamana Mahakamani. 

Ugonjwa wa Kipindupindu wahamia Mkoa wa Pwani… Manispaa ya Kindondoni imeagiza Polisi kukamata Mama Ntilie na Baba Lishe wanaokeuka agizo la kutokufanya biashara kwenye kipindi hiki. 

Watu 9 wa familia moja wapoteza maisha baada ya nyumba yao kuteketea na moto maeneo ya Buguruni Malapa jijini Dar es salaam… Mkazi wa Mwanayamala Dar es salaamafariki dunia baada ya kugonga kichwa cha treni… Mzambia akamatwa na kufikishwa polisi akiwa na kitambulisho cha kupiga kura na kuishi Tanzania kinyume na Sheria.
Unaweza kusikiliza uchambuzi wote wa magazeti kwenye sauti yake hapa chini.

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini