STAA Huyu Naye Aondoka Rasmi MANCHESTER UNITED

Kocha Louis van Gaal ameendelea kusafisha timu kwa kuuza wachezaji au kuwatoa kwa mkopo. Baada ya mchana wa leo kumtoa kwa mkopo Januzaj, jioni hii klabu ya Manchester United imemuuza mshambuliaji wake Javier “Chicharito” Hernandez.
  Mshambuliaji wa Mexico ameuzwa kwenda klabu ya Bayer Leverkusen na amesaini mkataba wa miaka 3 na klabu hiyo inayoshiriki ligi ya Ujerumani.
  Chicharito aliyejiunga na United kutoka klabu ya  Guadalajara kwa ada ya £6.9m mwaka 2010, ameuzwa kwenda Leverkusen kwa ada isiyopungua kiasi cha £8.75 million

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini