Je, Wajua? Q-Chief Kaandaa Wimbo Utakaotoka Siku Akifa!

Msanii nyota wa muziki nchini, Aboubakar Shaaban Katwila maarufu kama Q-Chief amesema kuna wimbo alioutunga kwa ajili ya mtoto wake utakaotoka baada ya kifo chake.
10956351_663821843741171_1618248528_n
Akizungumza na BBC Swahili hivi karibuni, Q Chief alisema aliamua kuandika wimbo huo baada ya mtoto wake huyo ‘kumtoa katika matumizi ya madawa ya kulevya.’
“Nilifanya ngoma ambayo inaitwa ‘Asante’, nilisema sita u-release labda Mungu akinichukua mbele ya haki itatoka,” alisema.
“Mtoto wangu alikuwa special sana wakati ule, maneno ya huo wimbo ni maneno yanayomhusia na yatabaki kwenye akili yake,” aliongeza.

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini