VITUKO VYA UCHAGUZI 2015: Mgombea Huyu wa UKAWA Atoa Mpya Kali Morogoro Mjini!

Dustan Shekidele, Morogoro
Vituko vya uchaguzi 2015! Mgombea wa nafasi ya udiwani kupitia Chama cha Wananchi (CUF) na Muunganiko wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), Kata ya Mji Mpya Manispaa ya Morogoro mjini hapa, Kondo Mkutu, ametoa kali ya mwaka baada ya kuwaita wake zake wawili jukwaani na kuwapatanisha.

Tukio hilo la kushangaza lilijiri mwishoni mwa wiki iliyopita kwenye mkutano wa ufunguzi wa kampeni uliofanyika katika Uwanja wa Kaloleni ambapo wahudhuriaji walihoji kwamba inawezekanaje mgombea wa siasa kuwapatanisha wake zake katika jukwaa la siasa na wakati sheria za umoja wa nchi zinazounda Jumuiya ya Madola (nchi zilizotawaliwa na Mwingereza), jambo hilo halitakiwi kufanyika jukwaani.

Mkutu anayetarajia kupambana vilivyo na mgombea kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wenslaus Kalogerezi aliamua kufanya hivyo ili kuwaoneshea wapiga kura kwamba kama ameweza kuwapatanisha wake zake wawili, Khadija Enzidoli (mke mkubwa) na Asia Kabwe (mke mdogo) basi hatashindwa kuwapatanisha wananchi wa Mji Mpya na kuwa kitu kimoja.

“Kama hili limewezekana, endapo mtanipa kura zenu katika uchaguzi wa mwaka huu, nitawaunganisha wananchi na kuleta maendeleo,” alisema.

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini