Deo Filikunjombe apata mpinzani Ludewa


Tume ya taifa ya Uchaguzi imelikubali pingamizi la aliyekuwa mgombea ubunge jimbo la Ludewa mkoani Njombe kupitia Chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA Msambichaka Batolomeo aliloliweka kupinga mgombea wa CCM Deo Filikunjombe (pichani) kupita bila kupingwa baada ya yeye kuenguliwa


Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na tume ya taifa ya uchaguzi NEC kupitia kwa mkurugenzi wa tume hiyo Kailima Kombwey wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, amesema baada ya kuikubali rufaa hiyo, imemrejesha mgombea huyo aendelee kugombea Ubunge wa Ludewa kupitia Chama chake cha CHADEMA


Pamoja na hayo pia tume hiyo imetolea matokeo ya rufaa mbalimbali za udiwani na ubunge zilizokatwa na wagombea mbalimbali nchi nzima

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini