Mchungaji wa kanisa mbaroni kwa mauaji Mwanza


MCHUNGAJI wa kanisa la Tanzania Adventist Conference (TACC) lililopo kata ya Kiseke, Ilemela mkoani Mwanza, Hanscolling Exaud (Munuo) anatuhumiwa ya Samwel Makoye.


Tukio hilo lilitokea jana saa 11 alfajiri wakati marehemu huyo ambaye alikuwa mchungaji wa ng’ombe alipoingia katika shamba la mtuhumiwa na kuanza kushambuliwa na mchungaji huyo wa kanisa kwa mpini wa jembe mwilini.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza, Kamishna Mwandamizi Msaidizi, Charles Mkumbo, amesema Makoye akiwa anakata majani aina ya matete kwa ajili ya kulishia ng’ombe, ghafla alivamiwa na Munuo na kuanza kushambuliwa hadi alipopoteza fahamu na mtuhumiwa huyo kukimbia.
Mkumbo amesema marehemu Makoye alifanikiwa kupiga kelele ambazo zilisaidia majirani kufika eneo la tukio, lakini kwa kuwa alikuwa hajiwezi kutokana na kipigo na alipoulizwa aliyemfanyia ukatili huo, alimtaja mchungaji Munuo.
“Baada ya wananchi kuelezwa hayo na marehemu ndipo walilitaarifu jeshi la polisi na kumpeleka hospitali ya Rufaa ya Bugando (BMC) kwa matibabu lakini alifariki saa moja baadaye,” amesema Mkumbo.
Kufuatia taarifa hizo, polisi walifanikiwa kumtia mbaroni mchungaji huyo na kukiri kumpiga mkata majani huyo ambaye ni mwajiri wa Holiday David, kutokana na kuvamia eneo la shamba lake kwa kukata majani ya ng’ombe.
Kamanda Mkumbo aliwataka wananchi kutojichukulia sheria mkononi kama alivyofanya mchungaji huyo ambaye atafikishwa mahakamani baada ya uchunguji kukamilika.

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini