Mauaji ya kutisha yatokea jijini Arusha

MAUAJI ya kutisha yametokea katika hotel ya kitalii ya A. Square Belmont maarufu kwa jina la A.M iliyopo katikati ya jiji la Arusha,baada ya mtu asiyefahamika wa jinsi ya kiume kukutwa amechinjwa kama kuku na kuondolewa viungo vyake kikiwemo kichwa ,viganja vya mikono na sehemu za siri.


Tukio hilo la kusikitisha limegundulika leo majira ya asubuhi na wahudumu wa hotel hiyo walipofika katika chumba alichokodi marehemu kwa lengo la 
kukifanyia usafi.




Taarifa zinadai kuwa marehemu alifika katika hotel hiyo agost 29 mwaka huu na kukodi chumba kimoja wapo gorofa ya pili na kulipia siku mbili zaidi
,hata hivyo juzi agost 30 aliongeza siku moja zaidi hadi tarehe agost 31.


Moja wa wahudumu katika hotel hiyo ambaye hakutaka kutaja jina lake alidai kuwa marehemu wakati anapatiwa chumba hicho alikuwa mwenyewe na kuandikisha jina moja akidai anatokea wilayani Karatu akifanyakazi ya Ualimu.


“Asubuhi ya leo mhudumu alienda kufanya usafi katika vyumba vya wateja na walipo fika chumba cha marehemu walijaribu kukifungua na kukikuta kiko wazi na walipo jaribu kuingia ndani ya chumba hicho ndipo walipoona mwili wa marehemu ukiwa utupu umelazwa kifudi fudi katika bafu la chumba hicho huku michirizi ya damu ikiwa pembeni ” alisema mhudumu huyo.


Aidha kufuatia tukio hilo uongozi wa hotel ulitoa taarifa kituo cha polisi 
na polisi walifika na kuchukua mwili huo hadi chumba cha kuifadhia maiti 
kilichopo hospitali ya mkoa Mount Meru.


Hata hivyo kabla ya kuchukuliwa mwili huo, polisi walitumia masaa matano kuwahoji wahudumu wa hotel hiyo kufanya uchunguzi wa kina zaidi kuhusiana na tukio hilo ,Uongozi wa hotel hiyo haukuwa tayari kuzungumzia tukio hilo na muda mwingi walionekana kujifungia katika vyumba maalum kukwepa waandishi wa habari


Kamanda wa polisi mkoa wa Arusha Liberatusi Sabasi alithibitisha tukio hilo 
na kueleza kuwa atalitolea ufafanuzi hapo baadae,Tukio hilo linahusishwa na ushirikina na hakuna anayeshikiliwa kuhusiana na tukio hilo na kwamba baada ya mauaji hayo wauaji waliondoka na nguo za marehemu pamoja na viungo vyake kikiwemo kichwa.



habari kwa mujibu wa libeneke la kaskazini blog

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini