LOWASSA Kuongeza JKT Vyuo Vya Ufundi

Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chadema, Edward Lowassa akihutubia umati wa wananchi katika kampeni zake zinazoendelea.
MGOMBEA Urais kupitia Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) kupitia Chama Cha Demokrasia (CHADEMA) Edward Lowassa amesema kuwa endapo atafanikiwa kuwa Rais atahakikisha vituo vya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) vinakuwa vyuo vya ufundi Stadi.

Aliyasema hayo mjini Mafinga wilayani Mufindi mkoani Iringa jana wakati wa mkutano wa kampeni kupitia umoja huo na kusema kuwa mara vijana watakapotoka hapo watakuwa na uwezo wa kujiajiri.

Lowassa alisema kuwa kipaumbele chake kikubwa endapo atachaguliwa atakachopigania ni pamoja na elimu mbalimbali ikiwemo ya ufundi ambayo ni rahisi kwa kijana kupata ajira ikiwa ni pamoja na kujiajiri wao wenyewe.

“Umefika wakati sasa kwa kuwekeza kwenye sekta ya elimu hususani elimu ya ufundi ambayo itawasaidia vijana kukabiliana na wimbi la ukosefu wa ajira,” alisema Lowassa. Aidha alisema kuwa elimu itagharimiwa na serikali kuanzia sekondari hadi chuo kikuu na anajua kuwa fedha za kuwasomesha wanafunzi kwa elimu za sekondari na chuo kikuu zipo.

Kwa upande wake aliyewahi kuwa Waziri Mkuu Frederick Sumaye alisema kuwa lengo kubwa la Ukawa ni kuhakikisha inapata majimbo mengi ya ubunge na udiwani ili waweze kuongoza halmashauri hapa nchini.

-HABARI LEO

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini