Licha ya Kudai Kumrudia Mungu! LULU Anaswa Akichetuka LIVE! Shuka Nayo Hapa...

vlcsnap-2015-08-26-10h08m22
Muigizaji Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ akiselebuka.
Musa Mateja
Msanii aliyejizolea umaarufu mkubwa kupitia fani ya uigizaji Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ amedaiwa kuchetuka upyaa licha ya hivi karibuni kudai kuwa amemrudia Mungu wake, Ijumaa lina mkanda mzima.

Tujikumbushe kwanza
Miezi kadhaa iliyopita, staa huyo alipokuwa akizungumza na mmoja wa waandishi wetu alisema kuwa, kutokana na kubaini kwamba amekuwa akimkosea sana Mungu, ameamua kubadili mfumo wa maisha yake na sasa ameamua kutembea na Yesu. 

“Sasa hivi popote ninapokwenda lazima niwe na Biblia. Hata katika kitanda ninacholala, ukibinua mto utakutana nayo. Ukweli ni kwamba katika kila ninachofanya ni lazima nisali kwanza. 

“Katika maisha tunayoishi na siku tulizonazo ni za uovu uliopindukia, nimegundua ni vyema kila ulipo uwe na utukufu wa Mungu kwa sababu hakuna anayejua siku wala saa ya kuondoka hapa duniani hivyo nawasihi watu wote kumjua Mungu,” alinukuliwa akisema Lulu. 

Ijumaa lamfungia kazi
Katika kuchunguza kama kweli amebadilika au ni manenomaneno tu, Ijumaa kwa muda mrefu limekuwa likimfuatilia usiku na mchana lakini halikuwahi kumnasa kwenye kumbi za sterehe na hata kwenye sherehe nyingi ambazo amekuwa akihudhuria alionekana kuwa ‘mtoto mzuri’.
Hata baadhi ya watu wake wa karibu wamekuwa wakimuelezea kuwa, mfumo wake wa maisha umebadilika sana kwani hata wale marafiki zake micharuko amewapotezea.
vlcsnap-2015-08-26-10h15m48“Kweli kabadilika, mara nyingi kwenye mikusanyiko anavaa kiheshima sana. Huwa namwambiaga twende klabu lakini amekuwa akinikatalia, amekuwa ni mtu wa Mungu,” alisema mmoja wa marafiki zake ambaye hakutaka jina lake liandikwe gazetini.
Alikuwa anazuga?
Hata hivyo, juzikati gazeti hili lilishitushwa na madai kwamba, staa huyo amerejea tena unywaji wa pombe, kujiachia kwenye kumbi za sterehe akiwa kavaa vivazi vyake vilee vya mapaja nje, mgongo wazi na kuvuta shisha.

Chanzo chetu cha kuaminika ambacho kipo karibu sana na staa huyo kilidai kuwa, Lulu sasa amerudia yale mambo yake ya zamani kwani juzikati alimuona kwenye ukumbi mmoja wa starehe akiwa na mademu wa mjini, mezani kukiwa na pombe na shisha.

“Mimi kwa kweli Lulu kanishangaza sana, amerudia tena yale mambo yake ya zamani, juzikati alikuwa kwenye ukumbi mmoja na mademu wa mjini ambao najua kwa kuwa nao karibu, tayari anamkaribisha shetani. Jaribuni kuzungumza naye jamani,” alisema sosi huyo huku akidai yeye amejaribu kuongea naye lakini anahisi hajamuelewa.

Kwenye Pati ya Rommy Jones
Katika kuthibitisha kile kinachosemwa, katika ‘bethidei pati’ ya DJ wa mwanamuziki Nasibu Abdul, ‘Diamond’, Rommy Jones, iliyofanyika hivi karibuni kwenye Ukumbi wa House Club uliopo Masaki jijini Dar, Lulu alikuwa mmoja wa waalikwa na alichokifanya kiliwashangaza wengi.

Kwenye pati hiyo, Lulu alionekana akinywa kinywaji kilichomchetua ile mbaya na hata ulipofika muda wa kucheza muziki, alijiachia kinomanoma.

Staili ya uchezaji wa Lulu ilionesha wazi alikuwa bwii kwani alikata mauno ya kufa mtu huku kigauni alichovalia kikipanda juu na kuacha mapaja yake wazi.
Kweli kachetuka upya

Mmoja wa watu waliokuwa ukumbini hapo alisema kuwa, kama kweli Lulu alikuwa akiwaambia watu ameokoka halafu anafanya mambo yale, atakuwa anamkosea sana Mungu.
“Duh! Ni Lulu huyu huyu aliyesema kaokoka kweli au namfananisha? Hata siamini, huenda alikuwa akizuga tu maana hawa wasanii wetu bwana, anakuambia kaacha pombe, kesho unamkuta bwii,” alisema shuhuda huyo.

Lulu anasemaje?
Katika kuishibisha habari hii, mwandishi wetu alifanya jitihada za kumtafuta Lulu ili kujua kulikoni anampa mwanya shetani, alipopatikana mahojiano yalikuwa hivi:

Kuna kipindi ulisema kila unapoenda uko na Biblia, hivi umeacha? Maana sasa hivi inadaiwa kuwa umerudia mambo yako ya zamani, pombe kwa sana, kuvaa vinguo vifupi? Hayo madai yana ukweli?
Lulu: Sijibu maswali ya aina hiyo na sitaki kusikia mnaniuliza kuhusu hizo stori zenu.

Ijumaa: Yamekuwa hayo, kinachokupanikisha ni nini sasa, si ujibu tu kama ni kweli au siyo kweli?
Lulu: Nimeshakuambia, ukitaka yachukue maelezo yangu ukiamua acha.

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini