KIMENUKA! Apple Music kuishtaki Tidal ya Jay Z kwa dola milioni 20, Drake ni chanzo!

New Look Wireless Festival 2015 - Day 1
Apple Music imetangaza vita kwa adui yake, Tidal ya Jay Z kutokana na Drake kutokea kwenye show ya kuchangisha fedha za wahanga wa kimbunga cha Katrina. 

Kwa mujibu wa mtandao wa Page Six, Tidal inaweza kukabiliwa na kesi ya kulipa dola milioni 20 kama nyimbo za Drake mwenye mkataba na Drake zilioneshwa kwenye mtandao wa Tidal. 

Wakurugenzi wa Apple Music hawakufurahishwa baada ya Drake alipothibitishwa kuwa atatumbuiza kwenye show ya Lil Wayne, Lil WeezyAna Fest ya mjini New Orleans jana usiku pamoja na show hiyo kuchangisha fedha kwaajili ya taasisi ya Tha Carter Fund inayosaidia miradi ya baada ya shule ya Louisiana. 

Wanasheria walihusishwa kwasababu tukio hilo lilikuwa likioneshwa live kupitia mtandao wa Tidal — na Drake ana mkataba exclusive na Apple Music wenye thamani ya dola milioni 19. 

Vyanzo vimedai kuwa kampuni hiyo imetishia kuishtaki Tidal kwa dola milioni 20 kama nyimbo za Drake zilioneshwa live kwenye show hiyo. 

Inasemekana kuwa kampuni hiyo iliwatumia Tidal barua kuwa Drake hatakiwi kuonekana live kwenye Tidal lakini barua ilipuuzwa. 

Nicki Minaj pia alitumbuiza kwenue show hiyo.
Vyanzo vimedai kuwa Jay Z na maofisa wa Tidal hawana namna zaidi ya kuondoa vipande anavyoonekana Drake.

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini