Zijue Faida Na Hasara za Kuongeza MAKALIO Kwa Njia Ya Upasuaji!

Kuna idadi kubwa sana ya wanawake duniani wanao hangaika kutafuta namna ya kuongeza ukubwa wa makalio yao pamoja na kutengeneza ama kurekebisha maumbile (shape) ya makalio yao.

Zipo njia mbali mbali zinazo weza kutumika kuongeza ukubwa wa makalio . Njia hizo ni pamoja na kufanya mazoezi maalumu ya kuongeza makalio na hips, kutumia dawa mbalimbali za kutengeneza makalio na hips pamoja na njia ya kufanyiwa upasuaji.


Katika makala yetu ya leo, tutaangazia suala la kuongeza na kutengeneza shape ya makalio kwa njia ya upasuaji.
Na katika hilo tutajikita katika aina ya upasuaji wa kuongeza ukubwa na shape ya makalio na hips unaotumika zaidi nchini Brazil ambao hujulikana kama Brazilian Butt Lift.

UPASUAJI WA KUONGEZA UKUBWA WA MAKALIO NI NINI ?
Ni aina ya upasuaji unao fanyika kwa ajili ya kuongeza ukubwa na shape ya makalio. Upasuaji huu ni lazima ufanywe na Daktari aliye thibitishwa katika fani ya upasuaji (Certified Surgeon)

AINA ZA UPASUAJI WA KUONGEZA MAKALIO.
Zipo aina kuu mbili za upasuaji wa kuongeza ukubwa wa makalio, ambazo ni :
1. KUPANDIKIZA SILICONE KWENYE MAKALIO : Hapa mpasuaji, hupandikiza silicone kwenye makalio kwa ajili ya kuyafanya yawe na muonekano mkubwa.

2. KUPANDIKIZA MAFUTA MAFUTA KWENYE MAKALIO; Hapa mpasuaji huhamisha mafuta yaliyo kusanywa katika maeneo mbalimbali ya mwili wako na kisha kuyapandikiza kwenye eneo la makalio na kuyafanya yawe makubwa

JINSI UPASUAJI WA KUONGEZA MAKALIO KWA NJIA YA KUHAMISHA MAFUTA YA MWILINI UNAVYO FANYIKA.
Kama tulivyo ona hapo juu, zipo njia kuu mbili za upasuaji wa kuongeza makalio ambazo ni njia ya kupandikizwa silicone na nyingine ni njia ya kuhamisha mafuta kutoka katika sehemu mbalimbali za mwili wako na kisha kuyapandikiza kwenye sehemu ya makalio na hivyo kuyafanya kubwa makubwa.

Hapa tutaangalia JINSI UPASUAJI WA MAKALIO KWA NJIA YA KUHAMISHA MAFUTA KUTOKA SEHEMU NYINGINE ZA MWILI NA KISHA KUYAWEKA KWENYE MAKALIO UNAVYO FANYIKA.

Hapa mpasuaji kwa kutumia teknolojia ya hali ya juu, atakusanya mafuta kutoka katika sehemu mbalimbali za mwili wako zenye mafuta mengi,kama vile kwenye mgongo, mikono, mapaja au tumboni na kuya safisha.

Baada ya kuyasafisha mafuta haya yatapandikizwa kwenye sehemu ya makalio yako eidha kwa njia ya sindano au kwa kuyasafirisha moja kwa moja hadi kwenye mishipa ya kwenye makalio yako na hivyo kuyafanya kuwa makubwa.

MTU MWENYE SIFA ZIPI ANAWEZA KUFANYIWA UPASUAJI WA AINA HII?
Kama nilivyo andika hapo juu, mpasuaji atakusanya mafuta kutoka kwenye sehemu mbalimbali za mwili wako na kisha kuyahamishia kwenye sehemu ya makalio. Hivyo basi unacho takiwa kuwa nacho ni mafuta ya ziada katika sehemu mbalimbali za mwili wako kama vile kwenye mapaja, mikono au tumboni n.k. Kama hauna mafuta ya kutosha katika sehemu nyingine za mwili wako, hauwezi kufanyiwa upasuaji huu.

Ili upasuaji huu uweze kukamilika,unatakiwa kuwa na kati ya sentimita za ujazo 250 hadi 350 za mafuta kwa makalio yote mawili.

2. KUPANDIKIZA MAKALIO KWA NJIA YA SILICONE.
Njia hii ya upasuaji, hutumiwa zaidi na wanawake wasio na kiwango kikubwa cha mafuta mwilini. Katika aina hii ya upasuaji, silicone hupandikizwa moja kwa moja katika sehemu ya makalio na hivyo kuyafanya yawe na muonekano mkubwa.

FAIDA ZA UPASUAJI KWA NJIA YA KUHAMISHA MAFUTA.
1. Upasuaji huu huchukua muda mfupi sana kukamilika, na kupona kwake huchukua muda mfupi pia. Unaweza kuendelea na shughuli zako za kila siku, baada ya wiki mbili tangu kukamilika kwa zoezi la upasuaji.
2. Kwa kuwa mpasuaji hutumia mafuta yako mwenyewe, hivyo kuna risk ndogo sana ya kupata maambukizi
3. Mafuta huchukua umbo la sehemu yalikopandikizwa, hivyo umbo lato litaonekana original. Hakuna atakaye weza kugundua kuwa umefanyiwa upasuaji.

HASARA ZA UPASUAJI KWA NJIA YA KUHAMISHA MAFUTA
1. Kwa kuwa mafuta yanahitaji mtiririko wa damu wa kutosha ili yaweze kuimarika, inashauriwa kutokuweka presha kubwa kwenye makalio yako kwa kipindi cha miezi miwili. Hivyo basi, hautakiwi kukaa kwa muda mrefu, pamoja na kutokuvaa nguo zinazo bana kwa muda wa miezi miwili.
2. Kwa sababu kudumu kwa mafuta yaliyo pandikizwa hakutabiriki, makalio yako yataongezeka kwa asilimia 25% hadi 50% na sio zaidi ya hapo.
3. Ili kuendelea kuongeza kiwango cha mafuta katika makalio yako, utatakiwa kuendelea kufanya upasuaji kila baada ya miezi mitatu.

UPASUAJI WA MAKALIO KWA NJIA YA SILICONE.
Upasuaji huu unafanyika zaidi katika nchi za magharibi. Katika upasuaji huu, silicone hupandikizwa chini kidogo ya eneo la mishipa ya kwenye makalio.

Upasuaji huu una hasara nyingi kuliko faida. Miongoni mwa hasara zitokanazo na aina hii ya upasuaji ni pamoja na kubabuka makalio, pamoja na kupatwa na kansa inayo weza kupelekea kukatwa na miguu. Maelfu ya wanawake waliotumia njia hii kuongeza ukubwa wa makalio yao, sasa wanajuta kwa kupatwa na madhara mbalimbali yatokanayo na upasuaji wa aina hii, kama vile kubabuka makalio yao pamoja na kukatwa miguu.

NJIA SALAMA ZA KUONGEZA UKUBWA WA MAKALIO : Kama wewe ni mdada wa kitanzania, na unataka kuongeza ukubwa wa makalio yako. Unaweza kufanya hivyo kwa kutumia njia salama. Zipo njia mbalimbali zinazo tumika kuongeza ukubwa wa makalio. Njia hizo ni pamoja na mazoezi ( ambayo huchukua kati ya miaka mitatu hadi saba kutoa majibu ) pamoja na dawa mbalimbali asilia, ambazo huchukua kati ya miezi mitatu hadi kutoa matokeo.

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …