AJALI: LORI LA MAFUTA LAANGUKA, WANANCHI WAJISEVIA MAFUTA
Ajali hiyo ya Lori la Mafuta lililokuwa likielekea Nchini Rwanda, imetokea Septemba 28,2014,eneo maarufu la Machinjioni-barabara ya Benaco - Rusumo wilayani Ngara mkoani Kagera ambapo chanzo chake ni kufeli mfumo wa breki.
Licha ya kujeruhi utingo mkononi na kuleta uharibifu wa barabara kwa mafuta iliyobeba ya diseli kumwagika,baadhi ya Wananchi walikosa uzalendo kwa kuiba mafuta yote yaliyokuwa katika tenki la lori hilo.