Kilichowakuta CHADEMA walioandamana Mwanza Sept.25
Kutoka 88.1 Mwanza ambapo Polisi wamekamata viongozi sita na wafuasi
kadhaa wa (CHADEMA) waliokuwa wakijiandaa kuandamana baada ya kukaidi
amri ya polisi kusitisha maandamano.
Ni September 25 saa 5.40 asubuhi muda mfupi baada ya wafuasi hao
kujipanga kwa maandamano yaliyokuwa yaanzie viwanja vya Sahara mpaka
ofisi za mkuu wa wilaya ya Nyamagana na kufanya mkutano mfupi wa hadhara
kufikisha ujumbe.
Purukushani ilidumu kwa zaidi ya dakika 120 ikiambatana na wafuasi hao
kupigwa virungu huku taarifa zisizo rasmi zikisema Polisi wamewatia
mbaroni watu 14 wanaodaiwa kuandamana bila kibali.
Kwa mujibu wa ripota wa nguvu Albert G. Sengo, licha ya kuthibitisha
kutokea kwa tukio hilo Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza bado halijatoa
taarifa kamili ambapo John Nzwalile katibu wa CHADEMA Mwanza amesema
>>> ‘naweza
kusema kwa ujumla tumefanikiwa, Polisi ndio wameandamana kwa wingi
kuliko hata sisi, tokea asubuhi ukienda chooni au kunywa chai Askari
kanzu wanakufatili, ukinywa chai na wao wanajifanya wanakunywa chai‘
‘Niseme maandamano yetu yamefanikiwa kwa sababu yalikua yamepangwa kwa
akili kubwa sana, tuliandamana kuanzia kichwani… hatukuandamana
ovyoovyo, hawakujua tunaanzia wapi tunaishia wapi…. tumeshangaa Polisi
wamekuja na vifaa utadhani unaangalia movie ya vita’
‘Mpaka sasa taarifa nilizonazo mwenyekiti wangu wa Nyamagana amekamatwa,
Katibu mwenezi Nyamagana, Mwenyekiti kata ya Bugogwa, Katibu wilaya ya
Ilemela wamekamatwa…. watu ambao kosa lao ni kuwaambia Watanzania kuna
pesa inaliwa na Wabunge kwenye batili la katiba’
‘Kwa kauli moja ya chama niseme tu kwamba maandamano na migomo isiyokua
na kikomo itaendelea…. tunazidi kujipanga vizuri kuangalia namna bora
zaidi ya kuandamana, tunataka watu wetu watoke Wanasheria wetu
wanajipanga…. kuhakikisha wanatoka bila masharti’