MASKINI KIJANA HUYU, ANUSURIKA KUUAWA KWA KUCHOMWA MOTO AKIDHANIWA NI MWIZI!


MTU mmoja aliyefahamika kwa jina la Richard Osward (40) mkazi wa Tabata Segerea, hivi karibuni alinusurika kuuawa kwa kuchomwa moto na wananchi baada ya kuhisiwa kuwa mwizi alipokutwa alfajiri akiwa na mfuko ambao ndani yake kulikuwa na bomba, huko Segerea.
Richard Osward aliyechomwa moto na watu wenye hasira kali akidhaniwa kuwa ni mwizi. Akizungumza kwa shida akiwa katika wodi namba 23 iliyomo ndani ya Jengo la Sewa Haji katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Richard alisema tukio hilo lilimkuta akiwa ameongozana na rafiki yake aliyemtaja kwa jina la Moses na kwamba walikuwa wakielekea Gerezani, Kariakoo ambako wanajishughulisha na ufundi wa magari.
Akiuguza majeraha ya moto katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili. “Nilitoka nyumbani nikiwa nimebeba bomba katika mfuko nikitaka kwenda kuliuza, tulipofika Segerea Seminari, tulisimamishwa na watu ambao walitutilia shaka wakaanza kutupekua. 
“Wakasema sisi ni wezi na hivyo lazima watuadhibu. Mara akapita dereva wa bodaboda ambaye alishinikiza kuwa sisi ni wezi na kutaka wachange hela wakanunue petroli ili watuchome moto, uzuri ni kwamba kwa kuwa ilikuwa usiku,wakashindwa kupata hayo mafuta,
lakini tunashukuru dada mmoja alikuja amevaa sare za kampuni moja ya ulinzi, akatukingia kifua na kusema watupeleke polisi na ndiyo tukafikishwa Kituo cha Polisi cha Stakishari na baadaye kunileta hapa kwa matibabu, kilichoniponza ni njaa lakini mimi ni mtu safi katika jamii, mwenzangu alifanikiwa kukimbia.”

Popular posts from this blog

Kocha mpya wa muda wa Chelsea kabidi awaambie ukweli mashabiki wa Chelsea, hii ndio kauli yake …

Walimu wadaiwa kuacha vipindi kukimbilia kufanya kazi migodini