ANGALIA PICHA PAKA AFUNGWA HIRIZI MTINI
Paka
mwenye hirizi kubwa shingoni akiwa amepigiliwa misumari juu ya mti
uliopo jirani na Msikiti wa kwa Mtawara uliopo Kata ya Mwembesongo,
Morogoro.
hali
isiyokuwa ya kawaida, paka mwenye hirizi kubwa shingoni akiwa hai
alikutwa amepigiliwa misumari juu ya mti uliopo jirani na Msikiti wa kwa
Mtawara uliopo Kata ya Mwembesongo mkoani hapa.
Tukio
hilo lililokusanya umati mkubwa wakiwemo waumini wa msikiti huo
lilitokea alfajiri ya Alhamisi iliyopita ambapo baadhi ya waumini wa
msikiti huo walikuwa wamefika msikitini kwa Swala ya Alfajiri.
Baadhi ya
waumini wa msikiti huo walipohojiwa na mwandishi wetu walisema alfajiri
hiyo walisikia sauti ya paka akilia kutoka kwenye mti huo uliopo
kandokando ya Barabara ya Mtawara inayoelekea Kichangani na Mji Mpya.
Watoto wakishudia tukio hilo la kushangaza.
“Tulifika
hapa msikitini kwa lengo la kuswali Swala ya Alfajiri kwa kuwa bado
kulikuwa na giza hatukuweza kumwona, lakini tulisikia akilia kwa kupiga
kelele mfululizo.
“Tuliposogelea
tulimwona akiwa juu ya mti huku amevishwa hirizi kubwa ya rangi nyeusi.
Haya ni mambo ya kishirikina, tena tuna wasiwasi hata wa maisha yetu.
“Unajua
eneo hili lina miti mingi lakini wahusika wamekuja kumpigilia misumari
paka huyu hapa. Mimi nasema wasakwe hawa watu tuwajue,” alisema muumini
mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Abdallah Said.
Umati wa watu wakishudia tukio hilo linalohusishwa na ushirkina.
Naye mjumbe wa kamati ya utendaji ya msikiti huo, Haji Said Dihole alipohojiwa na mwanahabari wetu alisema:
”Kama
kuna mtu alitaka kutujaribu angemuweka paka huyo kwenye eneo letu la
msikiti angeipata habari yake, pia nasikia tukio kama hili liko kwa
majirani wetu pale Kanisa la T.A.G Mwembesongo, nenda kashuhudie.”
Paka huyo baada ya kutolewa mtini.
Baaada ya
kupata taarifa hizo, mwandishi wetu alifunga safari hadi kwenye Kanisa
la Tanzania Assemblies of God ‘T.A.G’ linalofahamika kwa jina la Bethel
Revival Temple lililopo Mwembesongo.
Mwandishi
wetu hakumkuta paka lakini wananchi wa eneo hilo walipoulizwa walikiri
kuwepo kwa paka huyo kwenye mtaa huo lililopo kanisa hilo lakini
aliondolewa.
Baadhi ya wananchi wakimwangalia paka huyo kwa karibu zaidi.
Haikufahamika mara moja mtu aliyeamua kuweka paka hao kwenye maeneo ya jirani na nyumba za ibada alikuwa na malengo gani.